Zacharia Isaay (Mbunge Mbulu): Serikali iache kigugumizi ieleze wazi kuhusu ugonjwa wa kupumua unaomaliza watu wa Mbulu

Zacharia Isaay (Mbunge Mbulu): Serikali iache kigugumizi ieleze wazi kuhusu ugonjwa wa kupumua unaomaliza watu wa Mbulu

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Posts
9,006
Reaction score
14,536
Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Isaay ametaka Serikali ya Tanzania kueleza wazi kuhusu alichokiita ugonjwa wa kupumua ambao anasema unamaliza watu wa Mbulu.

Isaay amezungumza kwa hisia kali bungeni leo Alhamisi Februari 11,2021 akisema hawezi kuzungumzia mpango badala yake anaona bora azungumzie hali ya wananchi wake ambao kila mara anakwenda kuzika.

"Serikali iache kigugumizi jimboni kwangu watu wanakwisha Spika,nimechoka kuzika hata leo wanazika mtoto wa diwani wakati mwingine nashindwa kukuaga Spika kwenda Mbulu naamua kutoroka,"amesema Isaay.

Mbunge huyo anasema wanaopoteza maisha jimboni kwake magonjwa yao yanafanana ambayo ni tatizo la kupumua akihofia kuwa msimu wa baridi jimboni kwake utaendelea kuwaumiza.

"Jana nilikwenda hospitali ya hapa Benjamin Mkapa (Dodoma) kwa ajili ya kufanya vipimo lakini wakaniambia mitungi ya gesi imejaa, watu ni wengi sasa nimesema kama watu watanichukia basi lakini nimesema," amesema Isaay.

Mbunge huyo ameomba Serikali kuangalia namna ya kuboresha dawa za mitishamba ambazo ameeleza kuwa zinasaidia kwa kiasi kikubwa lakini akabainisha kuwa zinapatikana kwa gharama kubwa.
-----
Maoni Yangu
Tukipata wabunge watano jasiri kama huyu, Tanzania tutapona.

Juxi katibu mkuu Afya kasema ametembelea hosipitali zote hali ni nzuri. Hebu ona mbunge kaenda hosipitali anasema hali ni mbaya.
Hawa wataalam wana takiwa kunyongwa.
 
Hakuna serikali ya kumsikiliza huyo Mbunge maana Chama na Serikali wameamua watu wafe huku waking'ang'ania msimamo wa "Hakuna Corona". Serikali inadhani inafanya vizuri kuwa Manunda, lakini inapocheza na maisha ya watu inajijengea kutoaminika. Itasema nini iaminike wakati watanzania wanaona inavyocheza na uhai wao?
 
mbungepicc-data.jpg


Dodoma, Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Isaay ametaka Serikali ya Tanzania kueleza wazi kuhusu alichokiita ugonjwa wa kupumua ambao anasema unamaliza watu wa Mbulu.
Isaay amezungumza kwa hisia kali bungeni leo Alhamisi Februari 11,2021 akisema hawezi kuzungumzia mpango badala yake anaona bora azungumzie hali ya wananchi wake ambao kila mara anakwenda kuzika.

"Serikali iache kigugumizi jimboni kwangu watu wanakwisha Spika,nimechoka kuzika hata leo wanazika mtoto wa diwani wakati mwingine nashindwa kukuaga Spika kwenda Mbulu naamua kutoroka,"amesema Isaay.

Mbunge huyo anasema wanaopoteza maisha jimboni kwake magonjwa yao yanafanana ambayo ni tatizo la kupumua akihofia kuwa msimu wa baridi jimboni kwake utaendelea kuwaumiza.

"Jana nilikwenda hospitali ya hapa Benjamin Mkapa (Dodoma) kwa ajili ya kufanya vipimo lakini wakaniambia mitungi ya gesi imejaa,watu ni wengi sasa nimesema kama watu watanichukia basi lakini nimesema," amesema Isaay.

Mbunge huyo ameomba Serikali kuangalia namna ya kuboresha dawa za miti shamba ambazo ameeleza kuwa zinasaidia kwa kiasi kikubwa lakini akabainisha kuwa zinapatikana kwa gharama kubwa.
 
Anateruhusiwa kusema kuna corona ni Rais, makamu wa Rais ,waziri mkuu au waziri wa afya. Huyu mbunge wa CCM anamtafuta mungu maneno. Ila Bila corona kumgusa mmoja wapo hapo juu tanzania itaendelea kusema hakuna corona.
 
Sidhani kama huu mwezi utaisha kabla wote hatujaanza kuongea lugha moja. Inachokera wanafiki wanayojifanya sasa hivi kusema huu ugonjwa haupo tumeponywa na Mungu na Tanzania ni taifa teule watageuka nyuzi 180 na wataanza kuongelea tahadhari zote baada ya JP kutangaza hali ya hatari. Hii tabia inakera sana.

Hakukuwa na haja kusubiri watu wengi wafe na familia nyingi zipoteze wapambanaji wao kwa kuacha wazee na watoto mayatima ndio serekali ikubali kuhamasisha watu wachukue tahadhari. Sio lazima kuweka watu lockdown ila kama serekali atleast ingekaa kimya badala kuponda juhudi za kujikomboa na huu ugonjwa. Kweli kama kiongozi anasimama hadharani anasema watu wasivae barakoa na anasema sio lazima kuchukua hatua kutekeleza social distancing ni mbaya sana.

Hii kitu ikishapiga sehemu nyingi nyeti nawahakikishia mtaona ujinga wa kuchukua tofauti za kisiasa na kuziingiza kila mahali hadi kwenye mambo nyeti.

Kwani kuna hasara gani kama Taifa kupambana na ugonjwa hata kama mnaamini haupo? Ni wajinga waliosema bora nusu shari kuliko shari kamili? Au kinga ni bora kuliko tiba? Hii inanikumbusha ule msemo ni Bora mtu uamini Mungu yupo kisha ufe uende umkose kuliko kuamini na kujimwamabafai Mungu hayupo alafu ufe uende umkute.
 
Back
Top Bottom