Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ZAHANATI MPYA KUFUNGULIWA LEO KIJIJINI NYABAENGERE, KATA YA MUSANJA
Utoaji wa Huduma za Afya waendelea kuboreshwa ndani ya vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini.
Kata ya Musanja yenye vijiji vitatu (Mabuimerafuru, Musanja na Nyabaengere) haikuwa na zahanati hata moja - wanatembea umbali mrefu kwenda kupata Huduma za Afya kwenye Kata jirani ya Murangi
Vijiji viwili (Nyabaengere na Mabuimerafuru) vinajenga zahanati za vijiji vyao, na leo Kijiji cha Nyabaengere kinazindua utoaji na Huduma za Afya kwenye zahanati yake mpya.
Michango ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere:
(i) ujenzi ulianza kupitia Harambee ya Mbunge wa Jimbo kwa kukusanya michango na nguvu kazi za wanakijiji na viongozi wao
Mbunge wa Jimbo: saruji mifuko 100
Diwani na Wanakijiji: thamani ya michango yao ni takribani Tsh milioni 5 (Tsh 5m)
Wazaliwa wa Kijiji cha Nyabaengere wamechangia jumla ya Tsh 400,000 (laki nne)
(ii) baadae, Halmashauri yetu (Musoma DC ilichangia Tsh milioni 50 (Tsh 50m)
(iii) vilevile, Serikali Kuu ilichangia Tsh milioni 50 (Tsh 50m)
Huduma za Afya zinaanza kutolewa leo, na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu inayohitajika unaendelea.
Picha iliyoambatanishwa hapa:
Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere
SHUKRANI:
Wananchi ya Jimbo la Musoma Vijijini na viongozi wao wanaendelea kuishukuru Serikali yetu inayoongozwa vizuri na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuchangia fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya vijijini mwetu (Musoma Vijijini)
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P.O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Ijumaa, 6 Dec 2024