Zahanati na Hospitali za Iringa vijijini zinanuka rushwa

Zahanati na Hospitali za Iringa vijijini zinanuka rushwa

mrubwavwasy

Senior Member
Joined
Apr 14, 2021
Posts
138
Reaction score
229
Tafadhali mkuu wa mkoa na wilaya ya Iringa, fanya uchunguzi kwenye zahanati za vijijini haswa Pawaga zinanuka rushwa!

Baadhi ya wauguzi wamefikia hatua wanatoza wajawazito pesa kama hawana wanaandikia referral Iringa mjini wakafanyiwe operation kama kuwakomoa, watu wanalalamika hawana wakuwasemea, wengine wanaogopa hata kwenda clinic.

Kuna muuguzi anajulikana kabisa ana sifa ya kubaka wajawazito siwezi kumtaja kwa kulinda kibarua chake, fanyeni uchunguzi kijiji cha Pawaga kuna zahanati watumishi wametengeneza system yao ya rushwa bila aibu wala huruma.
 
Hawa wauguzi wa vijijin wanawatesa sana watu wa vijijin, sometimes hata kunakuwa hakuna maana kuwa na hivyo vituo vya afya huko vijijin
 
Kumbuka Mama alisema ukali si jambo jema. Enzi za Dkt Magufuli watu walifanya kazi sana
 
Wasilisha malalamiko haya kwa mkurugenzi,dc,diwani, n.k
 
siyo malalamiko, hii ni fact ...wakinamama wanateseka sana huko vijijin
Referral Ni kitu cha kawaida sana.

Na Hakuna hospital ya rufaa inayopokea tu mgonjwa yeyote hata asiye na complications zozote kwasababu tu eti kapelekwa kwa rufaa akanyiwe Caesar.

Pili ,Ni kweli Wajawazito Ni BURE lakini wale tu wenye kadi za Kliniki ( bila kadi utalipa )

Muhimu ili kukwepa rushwa, ukitoa pesa dai risiti ya MASHINE. Easy
 
Back
Top Bottom