John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Picha: kocha, Mwinyi Zahera
Mapema leo Jumatano Februari 23, 2022 uongozi wa Coastal Union ya Tanga ulikuwa na kikao cha kukamilisha dili hatua za mwisho ili kuwa kocha wao kuchukua nafasi ya Melis Medo ambaye ametimuliwa kutokana na matokeo mabaya.
Pande hizo zimekutana katika hoteli moja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumalizana, ikiwa ni mwendelezo wa mazungumzo yao waliyoanza Ijumaa iliyopita.
Hivyo, muda wowote kuanzia sasa Coastal watamtangaza kocha huyo wa zamani wa Yanga kuwa kocha wao mkuu hadi mwisho wa msimu huu.