Zahera na mashabiki wa Yanga hawajielewi

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Hata Jana Zahera amelalamika Simba wamepewa ubingwa, kumbukeni Yanga mechi zote round ya kwanza walicheza Dar wakawa wanaongoza, Simba ikiwa mikoani ikishinda na kukusanya points, wakati huo Yanga wapo kileleni, walipoenda mikoani kwenye viwanja vibovu ambavyo simba ilikuwa ikishinda wakaanza kupoteza mechi.


Head to head Yanga kapigwa na Simba msimu huu, wakati simba inacheza kimataifa yanga walikuwa wanasahau mechi zao na kuja uwanja wa taifa kushangilia wapinzani wa Simba.

Mechi zote tulizocheza na vilabu vya Congo mmepoteza mechi zenu za ligi kwa udhuru wa Zahera.

List ya wachezaji,
Makipa unaweza kufananisha kindoki na Manula au Dida?
Chama unaweza kumfananisha na Feisal/Ajibu au tshimbi? Okwi na Ngasa uwafananishe? Makambo Ni mzuri je ukimfananisha na Bocco, Tambwe utamfananisha na Kagere?
Boban utamfananisha na mkude ,Mzamiru au Kotei?

Mchezi anayeongoza kwa magoli yupo timu gani?mchezaji mwenye assist nyingi wa club gani.

Kama Yanga ni wazuri,Simba ilitolewa kwenye FA mda mrefu,huko nani alibebwa hadi mtolewe FA wakati Simba walishatolewa?.
 
mbeleko imefinya kazi.... ndo maana kambuzi hakachezeshi tena ligi kuu
 
Hawa Yanga kuna mental disturbance wanayo!! Tuwaache waongee wanavyotaka! Wafurukute watakavyofurkta, ila ubingwa tayr Simba kashabeba!!
Yanga kumbuken fadhila za Simba za kufika hatua waliofika kweny Klabu bingwa!! Umewapa na nyie nafas next sizoni!
Simba wanawapenda ndy mana wali-fight!!
 
Hakukosea TFF walimsimamisha kwa ajili ya malalamiko yenu ya kijinga
mbeleko imefinya kazi.... ndo maana kambuzi hakachezeshi tena ligi kuu
 
Hiyo favour nilidhani ni mwaka huu, hadi nilipoona Zahera analia machozi akihojiwa alipotolewa FA na lipuli
 
Zahera ni mjanja sana, anachofanya ni kucheza na akili za mashabiki wa yanga .Ashajua simba na yanga ndio timu zenye mashabiki wengi kwahiyo hataki kuongea ukweli kwa ajili ya kutetea kibarua chake!! Anajua alichowapromise mashabiki wa yanga na hiko kitu kikaenda kinyume!! So ana make excuses ili mashabiki wa timu ya yanga waone timu yao ilikuwa bora zaidi ya simba angali ukweli unajulikana!! Kwahiyo anachofanya ni kuwaaminisha mashabiki timu yake inaonewa nao kwakuwa wana mahaba yaliyozidi wanaamini hiko kitu!!
 
Mashabiki nao hawawezi, hata FA wameonewa?
 
Baadhi ya mashabiki wa Yanga na Kocha wao hawajielewi na wasahaulifu kabisa na ukiwaelewesha una poteza muda wako. Walipofungwa na Lipuli, Mtibwa na Stendi walisingizia Simba imehusika. Walipofungwa na Simba Kocha alizungumza na waandishi wa habari akasema wazi wazi kuwa wachezaji wa Simba wapo level ya juu na wana akili kuliko wa Yanga ndio maana Simba ikashinda mchezo ule. Mwisho wa ligi Zahera na baadhi ya mashabiki wanasema Simba kabebwa. Ausems kila aliposhindwa mechi alikubali matokeo na kusema ukweli kuwa anarudi kujipanga upya kwa ajili ya mechi inayofuata na matokeo yalionekana.

Zahera anacheza sana na akili za baadhi ya wanayanga. Anchozungumza wao wanamini hawajiulizi wakati mwingine ni ujanja tu wa Zahera kujitetea na kushindwa. Cha kuchekesha hao mashabiki hawajiulizi ni mfanyakazi gani duniani ambaye yupo tayari kufanya kazi bure bila kulipwa mshahara na bado anaendelea na kazi? Jibu ni Ajibu na Makambo na wengineo watakaoendelea kuuzwa.Wasichojua baadhi ya mashabiki wa yanga commission/ cha juu cha wachezaji wawili inaweza kuwa hata zaidi ya mshahara hasa ikiwa mchezaji kapata timu inayoeleweka na halafu mchezaji huyo mkataba wake umeisha; japo kwa Makambo mkataba haujaisha bado commission/ cha juu ni cha kutosha tu.

Yanga ilijiondoa kwenye mbio za ubingwa siku walipomfukuza Kakolanya badala ya kumsuluhisha na Zahera kwa maslahi mapana ya club. Ukichanganya na kikosi ambacho sio kipana kwa vyote vyote yanga ilitegemea ubingwa kwa bahati zaidi.

Lakini nategemea Dk. Msolla wakishirikiana na Mwakalebela watakuwa wa kweli na kuona shida ya Yanga ilikuwa wapi na watarekebisha mapungufu yaliyojitokeza ili waanze ligi ijayo kiushindani wakiwa na kikosi kipana zaidi. Pia Kocha asiwe mtu wa mwisho wa kumfukuza mchezaji badala yake awasilishe mashtaka kwa uongozi ili mchezaji naye asikilizwe isije ikawa chuki binafsi za kocha. Na pale timu itakaposhindwa uwanjani kwa ninavyomjua Dk Msolla hata tafuta visingizio rahisi rahisi kama Zahera badala yake atatafuta tatizo ni nini namna ya kulitatua hilo tatizo.
 
hakuna mshabiki yoyote wa mpira ambae hajui simba inabebwa, hata mtoto wa primary school anajua simba wamebeba ubingwa kwa kubebwa na marefa na kununua mechi
 
We Ni tahira unajulikana humu
 
hakuna mshabiki yoyote wa mpira ambae hajui simba inabebwa, hata mtoto wa primary school anajua simba wamebeba ubingwa kwa kubebwa na marefa na kununua mechi
We Ni tahira unajulikana humu
 
Makambo, Ajibu wamesajiliwa timu kubwa afrika kwa sababu kiwango chao ni cha juu kupita wachezaj wote kwenye ligi , hakuna cha okwi wala kagere
 
simba hawatafika robo fainali ya champion leagua tena milele, kwa mpira ule mbovu wa kubahatisha magol ya dakika za majeruhi, raundi ya kwanza tu out.
 
Makambo, Ajibu wamesajiliwa timu kubwa afrika kwa sababu kiwango chao ni cha juu kupita wachezaj wote kwenye ligi , hakuna cha okwi wala kagere
Tahira namba moja JF unafahamika
 
kama simba ni timu bora kwa nini hakuna mchezaji hata mmoja anaetakiwa na klabu kubwa za afrika, simba ni mkusanyiko wa magarasa na wazee
 
Simba ni timu kubwa, timu za nje zinaogopa bei za kina Kagere
kama simba ni timu bora kwa nini hakuna mchezaji hata mmoja anaetakiwa na klabu kubwa za afrika, simba ni mkusanyiko wa magarasa na wazee
 
Kagere ana miaka 44, mtoto wake ana mtoto anaitwa babu halafu ndio tegemeo la simba hahaha
 
Ismail Aden Rage, I salute you.

You know your people much better than anybody else.
 
Yanga walipoteza ubingwa pale zahera alipowaacha Yanga akabaki dar es Salaam yanga akapigwa na lipuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…