Zaidi ya bilioni 200 kutumika kutandaza mkongo wa Taifa wa mawasiliano wenye urefu wa 4244km kwa kutumia miundombinu ya TANESCO

Zaidi ya bilioni 200 kutumika kutandaza mkongo wa Taifa wa mawasiliano wenye urefu wa 4244km kwa kutumia miundombinu ya TANESCO

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
ZAIDI YA BILIONI 200 KUTUMIKA KUTANDAZA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO WENYE UREFU WA 4244KM KWA KUTUMIA MIUNDOMBINU YA TANESCO

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha zaidi ya bilioni 200 kwa lengo la kutandaza Mkongo wa taifa wenye urefu wa 4244Km kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO). Mradi huu utapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za huduma za Mawasiliano Tanzania na kufikisha huduma za intaneti kwa maeneo mengi Nchini kwa kutumia mradi unaojulikana kwa jina la "FIBER TO HOME kwa sababu Mawasiliano ni haki ya kila Mtanzania na lazima yafike Nchi nzima ". - Ameyasema hayo Mhe. Dr. Faustine Ndugulile Waziri wa Mawasiliano na technolojia ya habari wakati wa halfa ya utiaji saini Mkataba Kati ya Wizara ya Mawasiliano na teKnolojia ya habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Ujenzi wa Miundombinu ya Mkongo wa taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme. Leo jijini Dar es Salaam

IMG_20210907_145156_405.jpg

IMG_20210907_145156_345.jpg

IMG-20210907-WA0145.jpg

IMG-20210907-WA0146.jpg

IMG-20210907-WA0140.jpg

IMG-20210907-WA0142.jpg
 
Anasema "mradi huo utapunguza kwa kiasi kubwa gharama za huduma za maendeleo na kufikisha huduma za internet kwa maeneo mengi Tanzania " huku mnafungia YouTube na twitter sasa internet mnaimairisha kwa matumizi gani ,mna akili za kujifunika shuka na kujamba sijui unamkomoa nani hapo.
 
Kwani kwa sasa tatizo ni Penetration (uhakika wa kasi na access) au gharama ya hio access, Ukizingatia gharama ya hio access ni Wenyewe ndio wameiweka kwahio naona kama tunapigiana kelele tu na kufuja pesa za Umma
 
Kwa hili Mama Samia hongera kwa ubunifu.

wizara na taasisi zinakiwa kufanya kazi kama timu moja.

Tunasubiri Nina na vitengo vingine ikiwemo kitengo cha Passport wasainiane mikataba kusomana online ili kusiwe na haja ya mtu kubeba midocuments manually akishajaza online

Idara ya uhamiaji na NIDA wako wizara moja lakini hawasomani
 
Hawa mawaziri nawakubali sana. They are real ministerial materials. Maono yao ni'' nini tuwafanyie watanzania na sio nini watanzania watufanyie''. Miradi,mipango na sera zinazotekelezwa ina mwelekeo wenye manufaa mapana kwa taifa na hata mtu mmoja mmoja.
 
"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha zaidi ya bilioni 200 kwa lengo la kutandaza Mkongo wa taifa wenye urefu wa 4244Km kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO).

Mradi huu utapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za huduma za Mawasiliano Tanzania na kufikisha huduma za intaneti kwa maeneo mengi Nchini kwa kutumia mradi unaojulikana kwa jina la " FIBER TO HOME kwa sababu Mawasiliano ni haki ya kila Mtanzania na lazima yafike Nchi nzima ". -

Ameyasema hayo Mhe. Dr. Faustine Ndugulile Waziri wa Mawasiliano na technolojia ya habari wakati wa halfa ya utiaji saini Mkataba Kati ya Wizara ya Mawasiliano na teKnolojia ya habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Ujenzi wa Miundombinu ya Mkongo wa taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme. Leo jijini Dar es Salaa.


IMG-20210907-WA0157.jpg
 
Kwa hili Mama Samia hongera kwa ubunifu.

wizara na taasisi zinakiwa kufanya kazi kama timu moja. Tunasubiri Nina na vitengo vingine ikiwemo kitengo cha Passport wasainiane mikataba kusomana online ili kusiwe na haja ya mtu kubeba midocuments manually akishajaza online

Idara ya uhamiaji na NIDA wako wizara moja lakini hawasomani
Well said. Hata jana uzinduzi wa vituo vya huduma za pamoja uliofanywa na waziri mkuu hapo POSTA DAR una maono haya.
 
Good idea! TTCL hawana miundo mbinu ya kutosha ndo maana hata utandazaji wake ukaishia kwenye baadhi ya sehemu tu! Sasa sijui kuna technlojia ipi, lakini kama inawezekana kutandaza mkongo wa mawasiliano kupitia lines za TANESCO, na kwavile TANESCO imeenda hadi vijijini, basi usambazaji wake utafika mbali zaidi kuliko ilivyokuwa upande wa TTCL

Hata hivyo, interest yangu sio kushuka bei, kwa sababu I bet haitashuka lakini angalau huduma itaweza kupatikana hadi vijijini
 
Dar bado hatujaweza kuwa na hizo fiber optic connection kwenye makazi na maofisi. Tuanze kufanya tuache maneno maneno mengi na matendo kidogo au hakuna kabisa
 
Well said. Hata jana uzinduzi wa vituo vya huduma za pamoja uliofanywa na waziri mkuu hapo POSTA DAR una maono haya.
Maono ni Sawa na kusema tuko mbioni kufikia lengo mmmm hizo mbio zitakamilika lini? Hiyo ni political word ! ! It can mean next century!!! !
 
Nakushukuru kwa maono yako, lakini ili ufike kesho unahitaji maono. Haya yanayofanyika sasa kama vile kutia saini, kuzindua n.k.yametokana na maono.
 
Back
Top Bottom