Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Wananchi wa kijiji cha Kitanga katika wilaya ya Kasulu mkoani kigoma wamelalamika zaidi ya ekari elfu saba za mazao kuvunwa na watu wasiojulikana pamoja na nyumba zao kuchomwa kutokana na mgogoro uliosababisha pia kifo cha mtu mmoja.
Wamemwambia Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi,kumekuwa na mgogoro wa shamba hilo ambalo linamilikiwa na halmashauri ya wilaya kwa muda mrefu kati ya wafugaji na wakulima ambapo hivi karibuni mazao yaliyolimwa na wananchi mbalimbali yalivunwa usiku.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh.Dk. Angelina Mabula ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watu waliofanya uhalifu, huku mkurugenzi wa Halmashauri Godfrey Kasekenya akiahidi kushughulikia mgogoro huo.
Chanzo: ITV
PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana