Zaidi ya Milioni 900 Zakusanywa Wilayani Kakonko Katika Sekta ya Madini

Zaidi ya Milioni 900 Zakusanywa Wilayani Kakonko Katika Sekta ya Madini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

ZAIDI YA MILION 900 ZAKUSANYWA WILAYANI KAKONKO KATIKA SEKTA YA MADINI

Imeelezwa kuwa, katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2019 hadi 2023 jumla ya shilingi 924,685,884 zilikusanywa kutokana na madini yaliyozalishwa katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.

Hayo yamesemwa Agosti 30, 2024 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Aloyce John Mbunge wa Buyungu aliyetaka kujua kiasi cha fedha zilipopatikana kutokana na madini katika Wilaya ya Kakonko kuanzia Mwaka 2019 hadi 2023.

Akijibu swali, Dkt. Kiruswa amesema kuwa, Wilaya ya Kakonko ni miongoni mwa Wilaya zilizojaliwa kuwa na madini ya dhahabu nchini.

"Kutokana na madini yanayozalishwa Kakonko Shilingi 725,171,133.52 zilitokana na mrabaha na Shilingi 199,514,750.46 zilitokana na ada ya ukaguzi wa madini yaliyozalishwa kwa kipindi kinachorejewa" amesema Dkt. Kiruswa.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa, Madini mengine yanayopatikana katika Wilaya hiyo ni madini ujenzi aina ya mchanga, chuma, Shaba, makaa ya mawe na chokaa ambayo kwa sehemu yamechangia katika ujenzi wa barabara zinazounganisha Wilaya hiyo na maeneo mengine nchini.

Mkoa wa Kigoma umeunganishwa na wilaya nane, kakonko, kasulu, kibondo, uvinza, Buhigwe, Kusulu vijijini, Kigoma mjini na kigoma vijijini
 

Attachments

  • imageskmn.jpg
    imageskmn.jpg
    15.1 KB · Views: 6
  • images.jpg
    images.jpg
    9.3 KB · Views: 4
  • a1db5992-cfdf-444c-b43c-41dc24d0d28c.jpg
    a1db5992-cfdf-444c-b43c-41dc24d0d28c.jpg
    39.2 KB · Views: 4
  • GWOUbqqWsAM6NSc.jpg
    GWOUbqqWsAM6NSc.jpg
    149.9 KB · Views: 4
  • GWOUqk5XUAEG_UN.jpg
    GWOUqk5XUAEG_UN.jpg
    154.5 KB · Views: 4
  • GWOUqlBXwAEwmVn.jpg
    GWOUqlBXwAEwmVn.jpg
    170.1 KB · Views: 2
  • GWOUqk3XsAAbsxk.jpg
    GWOUqk3XsAAbsxk.jpg
    151.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom