#COVID19 Zaidi ya nusu ya Watu wazima wameshapata Chanjo kamili ya Coronavirus

#COVID19 Zaidi ya nusu ya Watu wazima wameshapata Chanjo kamili ya Coronavirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Umoja wa Ulaya umesema zaidi ya nusu ya raia wake watu wazima wamepatiwa chanjo kamili ya Covid-19, wakati nchi barani humo na Asia zikiendelea kukabiliana na maambukizi mapya yanayochangiwa na kirusi cha Delta.

Umoja wa Ulaya umesema watu milioni 200 wamepatiwa chanjo kamili, ikiwa ni nusu ya idadi ya watu wazima, lakini bado wameshindwa kufikia lengo la asilimia 70 hadi majira ya joto.

Kansela Angela Merkel amesema visa vya maambukizi nchini Ujerumani vinapanda kwa kiasi kikubwa. Ujerumani inaungana na nchi nyingine za ulaya, ambazo zimeshuhudia ongezeko la maambukizi ya Covid-19 katika wiki za hivi karibuni yanayochangiwa na kirusi cha Delta kilichogunduliwa mara ya kwanza nchini India.

Benki kuu ya Ulaya imesema wasiwasi juu ya wimbi la maambukizi inamaanisha kuwa milango ya fedha ya uokozi iko wazi ili kuhakikisha kuwa uchumi ambao ulikuwa umeanza kuimarika hauporomoki tena.

Mkuu wa benki hiyo Christine Lagarde ameonya kuongezeka kwa wasiwasi wa kiuchumi unaotokana na kirusi cha Delta wakati benki hiyo ikiuweka vizuri mfuko wake wa uokoaji uchumi kufuatia mkutano wa baraza la wanachama wake 25.


DW Swahili
 
Au hata chanjo haijui ifanye kazi gani, tunaambiwa huko ulaya idadi kubwa ya watu imechanjwa vilevile visa vipya vinazidi kuripotiwa, wengine tunashindwa kuelewa nguvu ya chanjo kwa huyo covid

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Au hata chanjo haijui ifanye kazi gani, tunaambiwa huko ulaya idadi kubwa ya watu imechanjwa vilevile visa vipya vinazidi kuripotiwa, wengine tunashindwa kuelewa nguvu ya chanjo kwa huyo covid

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Visa vingi vipya ni vya wale wasiochajwa.

Ndio maana baadhi ya nchi zimeanza kuweka utaratibu wa chanjo za lazima. Usipotaka chanjo 'potelea mbali' lakini utajikuta unaanza kutengwa na jamii.

Ukigomea chanjo, utakosa kibali cha kukusanyika na wengine katika maeneo mbalimbali, utakosa huduma mbalimbali za kijamii, utakosa baadhi ya ajira na kadhalika!
 
Back
Top Bottom