Serikali imeeleza kuwa imepanga kutumia zaidi ya shilingi trilioni sita kujenga kipande cha sita cha Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma.
View attachment 3632792
Akizungumza katika Kipindi cha Jambo Wikendi cha TBC 1, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Masanja, amesema kipande hicho ndicho cha mwisho katika ujenzi wa reli ya SGR inayounganisha Dar es Salaam na Mwanza pamoja na Kigoma.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha usafirishaji wa mizigo na abiria kwa haraka, kuongeza ufanisi wa huduma za reli na kupunguza gharama za usafiri.