Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Wananchi zaidi ya Laki moja wadaiwa kukosa haki yao ya msingi ya kupiga kura katika maeneo yao ndani ya Tarafa ya Ngorongoro Wilayani Ngorongoro badala yake inaelezwa kwamba wengine kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), wamepangiwa kupigia kura Msomera mkoani Tanga licha ya kutokuwa wakazi wa huko.
Wakizungumza Agosti 2,2024 mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha, waliojitambulisha kuwa wawakilishi wa wananchi hao wamedai kuwa wamesikitishwa na kitendo cha kunyimwa haki ya kupiga kura katika vituo vyao vilivyopo katika Tarafa ya Ngorongoro.
Akizungumzia hilo Dwani wa kata ya Oloitole iliyopo Tarafa ya Ngorongoro, James Moringe amesema kuwa amesikitiswa kwa uamuzi huo wa kunyimwa haki kupiga kura maeneo ya Ngorongoro na badala yake kupangiwa kupiga kura Kijiji cha Msomera mkoa wa Tanga wakati bado hawajahamia huko kwa hiari kama Serikali inavyodai.
Ameongeza kuwa wao kama Wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro wanailaumu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kuondoa vituo vyao vya kupigia kura katika chaguzi badala yake kupeleka majina yao katika Tarafa zingine na Msomera bila hiari yao.
Aidha Mwenyekiti wa Kijiji cha Bulati, Sabore Ngarus amesema kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi wa tarafa ya Ngorongoro ambao wanadai haki yao ya kupiga kura katika maeneo yao wanayoishi.
Amesema kufuatia orodha ya vituo vya kujiandikishia kupiga kura Nchi nzima iliyotolewa na INEC imeviondoa vituo vya kujiandikisha kupiga kura katika Kata kumi na moja (11) na vijiji ishirini na tano (25) ndani ya Tarafa ya Ngorongoro badala yake anadai wamepangiwa kujiandikisha katika Tarafa zingine pamoja na Msomera.
Bwana Sabore amebainisha kuwa tume imefanya kinyume na taratibu na ibara namba tano (5) ya tume huru ya uchaguzi ambayo inampa kila mtanzania haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Itakumbukwa Serikali kupitia kauli za vingongozi mbalimbali ikiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na vingozi wengine wamekuwa wakisikika kuwa wananchi katika eneo hilo wanaohama wanaondoka kwa hiari na kuwa wanaobaki hawalazimishwi kuhama.
Soma: Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673
Lakini kumekuwepo na mwendelezo wa taarifa zinazodai kuwa baadhi ya huduma zimekuwa zikisitishwa kwa wakazi waliobakia eneo hilo kinyume na ilivyokuwa awali kabla mchakato wa kuhama haujaanza.
Pia Soma
~ Wamasai wa Ngorongoro watoa tamko kunyang'anywa haki ya kupiga kura 2024 na 2025
~ Njama: Vituo vyote vya kupigia kura Jimbo la Ngorongoro vimefutwa, ila watu bado wapo na Jimbo bado lipo