Kiukweli hakuna mtu ambaye yuko salama mtandaoni. Awe ni mtaalamu wa ICT au mtu wa kawaida, maadam tu anatumia vifaa ambavyo hajavitengeneza yeye. Hata mitandao mingi tunayotembelea inahusika mno na kutudukua na kufuatilia tunafanya nini mtandaoni.
Binafsi kudululiwa siogopi kwasababu sina la kuficha. Eti nianze kuhangaika na VPN kisa tu naogopa mitandao nayotembelea itafuatilia na kufahamu kwamba nimetoka kutembelea tovuti za ngono au mawasiliano yangu yakoje na watu. Huu mzigo wa kutoyaishi maisha yangu kisa kumuogopa mtu nisiyemfahamu siwezi kuubeba.
Japo binafsi, naona hakuna tabia ya kishenzi kama kudukua taarifa za mtu mtandaoni, kama wewe hauko kwenye taasisi za usalama ambazo zimepewa mamlaka kufanya hivyo kwasababu ya usalama. Yaani ni tabia ya kishenzi mno.