Zainab Katimba: Serikali Kutoa Waraka Kwaajili ya Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Serikali inatarajia kutoa waraka utakao waelekeza wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutekeleza miongozo inayowahusu watumishi wa Umma wenye ulemavu ili wapate mazingira rafiki na wezeshi wanapotekeleza majukumu yao.

Kauli hiyo imetolewa Februari 06,2025 Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zaina Katimba alipomwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa katika ufunguzi wa kikao cha wajumbe wa baraza la Taifa wa Chama cha Walimu Tanzania ambao ni wawakilishi wa walimu wenye Ulemavu.



“Serikali itatoa waraka kuwakumbusha wakurugenzi wote nchini kutekeleza miongozo inayowahusu watumishi wa umma wenye ulemavu na niziombe taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa kuendelea kufanikisha upatikanaji wa vifaa visaidizi kwa watumishi wa umma na wanafunzi wenye ulemavu” Amesema

katika hatua nyingine Mhe. Katimba amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa kutoa nafasi kwa watu wenye Ulemavu wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili waingie kwenye vyombo vya maamuzi kwa ustawi na maendeleo ya watu wenye ulemavu na taifa kwa ujumla.

 

Attachments

  • GjIPaPdXcAAnFHM.jpg
    111.8 KB · Views: 1
  • GjIPbbVXoAEHTfj.jpg
    117 KB · Views: 1
  • GjIPbbTXgAAEI4b.jpg
    138.4 KB · Views: 1
  • GjIPbbNXEAAfgwA.jpg
    140 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…