Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wahusika watakaotembelea watapata elimu ya Afya ya Akili ili kuweza kujua namna ya kujilinda vyema na kufikia malengo yao.
Mkurugenzi Mkuu wa ZAMHSO, Mwalimu wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Abdurahman Al-Sumait, na Mwanasaikolojia kutoka Hospitali ya Ampola Tasakhtaa, Zaituni Shabani Salum, alisema:
“Leo tumekuwa na siku yenye mafanikio makubwa katika kuendelea kueneza elimu ya Afya ya Akili Shuleni! 📚💙 katika Skuli ya Aboud Jumbe, tumeweza kushiriki maarifa muhimu kuhusu Afya ya Akili na ustawi wa Wanafunzi, tukihakikisha kila mmoja anapata uelewa sahihi wa jinsi ya kujali afya yake ya kiakili.”
“Tutapumzisha zoezi letu la utoaji wa elimu kwa muda wa wiki 3 ili kuwapa nafasi Wanafunzi wetu wa chuo ambao ndio watoaji wakuu wa elimu kwa ajili ya mitihani yao ya UE inayotarajia kuanza Februari 11, 2025, kisha baada ya hapo tutakuwa na safari ya Iringa.
“Tukirudi tutaendelea na mradi wetu mwezi Machi, Mungu akipenda kama ratiba yetu inavyooneka kwenye page zetu. Tunatoa wito kwa wote ambao wapo tayari kutudhamini wa wasiliane na sisi.”
Mradi huu wa miezi sita unategemea kuhitimishwa mwishoni mwa mwezi Juni 2025, kabla ya kuendelea na awamu yake ya pili kisiwani Pemba kuanzia Agosti hadi Desemba 2025.
Pia soma:
~ Zanzibar Mental Health Support Organization imeanza kutekeleza Rasmi Mradi wa Elimu ya Afya ya Akili Shuleni
~ ZAMHSO: Mradi wa Afya ya Akili Shuleni utaacha athari chanya na kuleta mabadiliko ya kudumu