Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 22,719
- 40,739
Hakuna kitu kilichowahi kuniumiza moyo kama nilipomuona mnyamwezi mwanzangu Ismal Aden Rage akilia kama mtoto baada ya KUTENDWA na APR.
Kwa kweli huu ni mkasa ambao wana simba wanabidi waujue na waje kwa wingi Chamazi kuungana na sisi kumlipia kisasi gwiji wao huyo.
Ilikuwa mwaka 2012 baada ya mashindano ya Kombe la Kagame. APR walikuja na mchezaji wao aliyeitwa Mbuyu Twitte, mnyarwanda mwenye asılı ya DRC.
Twitte alionesha uwezo mkubwa sana na baada ya mashindano Simba ikahitaji huduma yake.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, akasafiri hadi Kigali kuonana na maafisaa wa APR ili wafanye biashara ya mchezaji huyo.
Wakaelewana, na wakampa ruhusa ya kuongea na mchezaji. Naye akaelewana naye, na akampa dola 30,000 na anapiga naye picha (ya juu kushoto) kama kiashira cha kwamba kazi imekwisha.
Rage akaituma picha nyumbani Tanzania ili itembee kwenye mitandao ya kijamii…na kweli picha ikatembea sana.
Kumbe APR hawakuwa wakweli kwa Rage. Twitte hakuwa mchezaji wao bali alikuwa klabuni hapo kwa mkopo akitokea FC Lupopo ya DRC.
Yanga wakapewa hizo taarifa na wakamtuma mafia wao mmoja hadi Lubumbashi, akakutana na maafisaa wa Lupopo na kufanya biashara ya mchezaji huyo.
Siku anakuja hapa nchini, akavalishwa jezi ya Yanga yenye namba nne na jina la Rage. Haya yalikuwa matusi makubwa sana kwa kiongozi huyo mtaalamu wa sheria.
Akaangua kilio kama mtoto mdogo akimlilia mchezaji huyo kiraka. Kama APR wangekuwa wakweli, Rage asingedhalilika namna ile, asingelia namna.
Sasa APR wamejileta wenyewe Azam Complex, wanasimba njooni tushirikiane kulipa kisasi.
Kiingilio ni cha mwananchi wa hali ya chini kabisa kwa hisani kubwa ya Azam Pesa.
VIP A ni shilingi 20,000 kama utanunua tiketi kwa Azam pesa. Ukinunua kwa pesa taslimu ni shilingi 22,000.
VIP B ni shilingi 10,000 kama utanunua tiketi kwa Azam pesa. Ukinunua kwa pesa taslimu ni shilingi 12,000.
VIP C ni shilingi 5,000 kama utanunua tiketi kwa Azam pesa. Ukinunua kwa pesa taslimu ni shilingi 7,000.
Mzunguko ni shilingi 3000 kama utanunua tiketi kwa Azam pesa. Ukinunua kwa pesa taslimu ni shilingi 5000.
Tumeipata Code. Tukutane Jumapili!
©️ Zakazakazi.