Kibunango na kundi lako nadhani hamkuwa mna elewa nataka nini .Unajua ukiwa umejiandaa kubisha kila kitu kwa ushabiki unakuwa mpuuzi na hata huwezi kuelewa maandiko.
)kuna daktari mmoja hivi wa mazingira kule morogoro(nikipata jibu nitawaambia
Mwaka 1992 sehemu ya Loliondo(LGSA) ilikodishwa kwa asasi ya uarabuni kwa ajili ya uwindaji na ubebaji wa wanyama kwa kipindi cha miaka 10. Mwaka mmoja baadae (1993) Waziri wa utalii wakati huo Abubakar Mgumia alijiuzuru kutokana na kashfa ya LGSA...
Sasa huyo Meghji anahusika vipi na hili... Hebu fafanueni
Dr. J Ngasongwa alijiuzuru uwaziri wa Utalii mwaka 1996 na baada kasi ya skandali ya loliondo na issue nyingine huko kwenye mbuga za wanyama kuongezeka aidha hakutiwa hatiani katika kushiriki kwenye skandali hiyo na ndio maana Mkapa akampa wizara nyingine baada ya kujiuzuru kwake.Kibunango
hivi hii kashfa ya Abubakar mgumia ni tofauti na ile iliyoibuliwa kuhusu Loliondo ikamfanya Dr.Juma Ngasongwa ajiuzulu?Nakumbuka kujiuzulu kwake kipindi cha mkapa ilimhusisha kumuuzia mwana wa mfalme wa nchi za kiarabu kipande cha mbuga.
Dr. J Ngasongwa alijiuzuru uwaziri wa Utalii mwaka 1996 na baada kasi ya skandali ya loliondo kuongezeka aidha hakutiwa hatiani katika kushiriki kwenye skandali hiyo na ndio maana Mkapa akampa wizara nyingine baada ya kujiuzuru kwake
Z. Meghji alianza uwaziri katika wizara ya Afya kama sikosei na tokea hapo akaenda Utalii kabla ya kuwa waziri wa Fedha..Mkuu Kibunango
Rekodi yangu inaonyesha Bi. Zakia Hamdani Meghji amekuwa waziri kwa kipindi hiki:
1994 -2005: (Minister) Ministry of Natural Resources & Tourism
2006 - 8/2/2008: (Minister) Ministry of Finance
Tuendelee!
Savimbi huyu mama kaingia wizara ya MALI YA ASILI 1997.Mkuu Kibunango
Hebu jaribu kucheki vizuri rekodi zako, sijui zangu ndiyo zitakuwa na makosa ama zako ndiyo zitakuwa na makosa maana hapa hatugombani ila tunawekana sawa katika kupata ukweli.
Rekodi yangu inaonyesha Bi. Zakia Hamdani Meghji amekuwa waziri kwa kipindi hiki:
1994 -2005: (Minister) Ministry of Natural Resources & Tourism
2006 - 8/2/2008: (Minister) Ministry of Finance
kwa hiyo nachanganyikiwa kidogo unaposema Dr. J. Ngasongwa alijiuzuru uwaziri wa utalii mwaka 1996: wakati mwaka 1996 kwa rekodi zangu tayari wizara ilikuwa mikononi mwa Mama Meghji.
Tuendelee!
Jamani, hivi huyu mmama anakanyagwa na nani,nana anamchukua huyu mama. naelewa kuwa mmewake alishakufaga. au anachukuliwa na fisadi mmoja hivi. naombeni nambieni mme wa huyu mama. ila siamini kama Rostam ndo anaemkanyaga.kama ingekuwa hivyo, basi tungesema yuko kwenye mfereji wa makambare yanayotisha, yanayotakiwa kuendewa na msumeno, sio kiwembe.
Kuna haja ya kuulizia hao ambao wanahusika na ukusanyaji na uandikaji wa CV za Wabunge wetu... Kwani hii hapo juu ni upotoshaji mkubwa wa habari na ni uzembe wa hali ya juu kwa asasi hiyo muhumi(Ofisi ya Bunge).Mkuu Kibunango
Asante kwa maelezo,
Basi hizi source za serikali nazo zinapotosha ama hajiandaliwi kitaalamu
hebu check hii
Zakia H. Meghji
Ministry of Natural Resources & Tourism Minister 1994 2005
Dr. Juma A Ngasongwa
Ministry of Natural Resources and Tourism Minister 1995 1996