Kuondokana na tatizo la unafiki and improving our IQ &EQ.Iko hivi, utakuka mtu amekosea na anahitaji kurekebisha alipokosea lakini mtu huyo anabagua aina ya watu wa kumwambia ukweli.
Hii ipo kuoanzia ngazi za familia, jamii na kitaifa. Kwa mtu binafsi, kiongozi au taasisi.
Unaweza kuthubutu kwa kujikaza kumweleza mtu madhaifu fulani, ila uwe tayari kukutana na kauli kama vile "huo ni wivu tu, anatamani hii nafasi angepewa yeye, ana chuki.
Na kama huyo kiongozi ni wa dini tofauti na yako basi utasikia suala la udini. Swali ni je, tutaweza kufika tunakotarajia kufika pasipo kurekebishana au kukosoana?
Mods wanafuta nyuzi , wana zinhide thread zisionekane na wengine imekuwa ni ovyo sanaSijapenda mods kuiondoa hii hoja kwenye jukwaa la siasa. Labda niwaambie, tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, si kila member atakuwa tayari kumzungumzia kiongozi au viongozi fulani moja kwa moja.
Wakati mwingine tutatumia lugha za mifano,visa au mikasa ili kufikisha ujumbe.
Leo hii kila anayetaka kuzungumzia madhaifu ya serikali lazima ajiandae kupingwa hata kama anachoeleza ni sahihi. Hoja ya jinsi, itikadi za dini,ukanda, utaifa, kiwango cha elimu, nk, zimekuwa zikitumika kudhoofisha hoja zinazokosoa serikali. Hivyo, tunaweza kutumia mifano, visa au mikasa.
NB: Akili kubwa hujadili zaidi hoja. Tujikike zaidi kwenye hoja