Makene
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 1,475
- 282
miongoni mwa mambo nisiyoweza kuelewa ni nadharia ya mageuzi. Nadharia hii ya kisayansi naiona kama jambo lililopitwa na wakati. Katika nyakati hizi za maendeleo ya kisayansi tuliyofikia haiingii akilini kuendelea kufikiri kuwa jamii ya aina binadamu ilitokana na jamii ya viumbe nyani.
Kama hivyo ndivyo ilivyo mbona hakujatokea jamii nyingine iliyo kati ya nyani na binadamu? Na hatuoni badiliko toka jamii binadamu kuelekea kiumbe kingine bora kuliko jamii ya sasa ya binadamu.
Mi naona nadharia hii kuwa ya kiwendawazimu kabisa.
Kila jamii inaendelea kuwa kama ilivyokuwa karne na karne. Tofauti za mambo madogo ya kimaumbile na tabia zinatokea kwa jinsi jamii hizi zinavyofanya jitihada ya kuendana na mazingira zinazojikuta zikiwemo, lakini si mabadiliko kuelekea kuwa kuwa jamii tofauti.
Kuamini nadharia hii ni sawa na kukubali jibu la mtoto anayesema akikuwa angependa kuwa tembo, tokana na kukosa ujuzi.