Zamaradi ataja ujio wa filamu yake aliyoiandaa kwa Milioni 200

Zamaradi ataja ujio wa filamu yake aliyoiandaa kwa Milioni 200

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2016
Posts
602
Reaction score
1,459
Dada Zama muda huu anaongea na Waandishi wa habari kasema kuwa kuna ujio wa filamu yake yenye mapigano ndani ambayo ameiandaa kwa millioni miambili
====

Mtangazaji maarufu nchini Tanzania, Zamaradi Mketema amekuja na filamu iliyomgharimu Sh200 milioni katika kuitengeneza huku akieleza kuwa filamu hiyo imekuja kuleta mapinduzi katika sekta ya filamu.

Filamu hiyo inayoitwa 'Cop's Enemy' aliyoanza kuitengenezwa tangu mwaka 2016 na prodyuza John K, imechezwa katika nchi tatu ikiwemo Tanzania, Australia na India.

Wakati wasanii walioshirikishwa wamo Wema Sepetu, Stanlenley Msungu na Aunt Ezekiel kutoka Bongo, Van Vicker wa Ghana na wengine kutoka Nigeria, India na Australia.

Zamaradi ambaye aliwahi kuongoza filamu ya Kigodoro Kantangaze na Nzowa, akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 4, 2019 amesema utengenezaji wa filamu hiyo ya gharama umelenga kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu hapa nchini ambayo imeonekana kushuka.

Amesema kutokana na hilo hakuhofia gharama watakazotumia kwani shida ilikuwa wafanye kitu kizuri kitakachorudisha heshima ya filamu nchini Tanzania.

Kwa upande wa waongozaji yupo Neema Ndempayo na John K kutoka nchini Australia ambaye pia ni mmoja wa wahusika katika filamu hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo sifa ni ipi?
Million 200?
Kuita waandishi?
Au kutengeneza movie?

Ngoja itoke tuone reviews, Bongo fleva huwa video zao wanaongeza sifuri moja kwenye gharama.

Hiyo movie ikiwa hata ya 70mil lazima itakuwa nzuri. Shida itakuja kwenye soko la ndani, atarudisha?

Natarajia kuona wasanii wa nchi kama Nigeria, Ghana na South ili kuliteka hilo soko na movie iende nje zaidi.
 
hahaha umeniwazia nn mpaka umeniuliza ilo swali Mkuu!!!!

Umetaja mil 200 kama pesa ndogo sana (vichenji).

Nikafikiria tu kama utakuwa na bal ya 1% ya hiyo hela kwenye account ya matumizi, obvious utakuwa na deals ambazo hiyo hela haikutishi hata kama haifiki lakini si haba.
 
Umetaja mil 200 kama pesa ndogo sana (vichenji).

Nikafikiria tu kama utakuwa na bal ya 1% ya hiyo hela kwenye account ya matumizi, obvious utakuwa na deals ambazo hiyo hela haikutishi hata kama haifiki lakini si haba.
Hapana mkuu!!! Sijafikisha. Lakini napambana.
 
Huyu Dada nae tangu aachane na ruge amekuwa mtu wa drama sana sijui ana tatizo gani?
 
Back
Top Bottom