Zambia: Aliyeachilia Wafungwa 13 akiwa amelewa Akamatwa

Zambia: Aliyeachilia Wafungwa 13 akiwa amelewa Akamatwa

Bakalalwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
748
Reaction score
1,217
Afisa wa Polisi Nchini Zambia, Titus Phiri, amekamatwa kwa madai ya kuwaachia huru Wafungwa zaidi ya kumi na tatu ili kusherehekea usiku wa Mwaka Mpya haliyakuwa amelewa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi la Zambia Phiri ambaye ni Mpelelezi wa ngazi ya Inspekta, ametuhumiwa kuchukua funguo za seli kwa nguvu akiwa katika hali ya ulevi kisha kufungua seli za Wanaume na Wanawake na kuwaambia Watuhumiwa kuwa wako huru kuingia mwaka mpya.

Mpaka sasa msako mkali unaendelea kuwatafuta Wafungwa 13 waliotoroka, miongoni mwao wakiwa ni wale wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya unyang’anyi na shambulio.

Aidha Jeshi la Polisi la Zambia limeeleza kuwa litaendelea kushikamana na maadili ya sheria na kuhakikisha kuwa hatua kali zinachukuliwa dhidi ya Maafisa wa Polisi watakaobainika kutumia vibaya mamlaka yao au kwenda kinyume na sheria.
#MillardAyoUPDATES
1735927838806.jpg
 
Ukiwa umelewa afya ya akili inakwenda mortuary
Kwa hiyo inabakia akili njema kwa wakati huo.Kwani shida ya akili ni msongo wa mawazo,upandapo juu ya meza misongo inayeyuka na kupotea angani.Ila pale unapopanda juu ya meza kwa kiasi kwa lengo tu la burudani binafsi.
 
Watuhumiwa walikosa uhaminifu,jamaa aliwaambia waupokee mwaka mpya...wangeupokea then warudi ndani.

Jamaa kalogwa huyo ,Kuna mtu alimbambikizia kitu sio Bure.
 
Jamaa alikubaliana nao kiroho safi wakasherehekee mwaka mpya kisha warudi kolokoloni ila wamemsaliti mwana,

Hawajafanya fare kabisa..
 
Back
Top Bottom