Zambia: Ofisa wa polisi mbaroni kwa kuwafungulia watuhumiwa washerehekee mwaka mpya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Ofisa mmoja wa polisi nchini Zambia, Titus Phiri amekamatwa kwa kosa la kulewa akiwa kazini na kuwaachia huru watuhumiwa 13 na yeye mwenyewe kukimbia.
IMG_2206.jpeg

Watu hao walikuwa wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi, ujambazi na mashambulizi.

Msemaji wa Polisi, Rae Hamoonga amesema Desemba 31, 2024 katika Kituo cha Polisi cha Cheelo jijini Lusaka, Inspekta Titus Phiri aliyekuwa amelewa, alichukua kwa nguvu funguo za vyumba husika kutoka kwa askari mwingine.

Kisha, inspekta huyo aliwafungulia watuhumiwa huku akiwaambia, "mpo huru kwenda kuupokea mwaka mpya".

Kati ya watuhumiwa 15, waliotoroka ni 13 na msako wa kuwatafuta unaendelea.

Soma, Pia:

Zambia: Waganga wakamatwa kwa jaribio la kutaka kumroga Rais Hichilema

Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu azuiliwa kugombea tena Urais uchaguzi wa mwaka 2026
==

A police officer in Zambia has been arrested for allegedly releasing over a dozen prisoners so they could celebrate New Year’s Eve.

Detective Inspector Titus Phiri “forcibly seized cell keys” on Tuesday morning whilst “in a state of intoxication,” Zambia’s Police Service said in a press release on Wednesday.

“Subsequently, (Phiri) unlocked both the male and female cells and instructed the suspects to leave, stating they were free to cross over into the New Year,” the police statement said.

A manhunt has been launched for 13 detainees who remain at large, according to the police statement. Some had been facing allegations of assault and theft among other crimes, it said.

“The Zambia Police Service reiterates its commitment to upholding law and order and assures the public that decisive action will be taken against any officer found to be abusing their authority or acting contrary to the law,” it added
 
Mwaka mpya umeanza na Mengi hakika.

😆😆!!
 
"mpo huru kwenda kuupokea mwaka mpya".- Mamlaka matamu aisee.
 
Hii nayo kali...!
TBT: Mwaka 1979 wakati vita ya Kagera imepamba moto, Mkuu wa Gereza fulani kule Bukoba aliwafungulia wafungwa ili kila mmoja ajiokoe nafsi yake!
 
Ofisa mmoja wa polisi nchini Zambia, Titus Phiri amekamatwa kwa kosa la kulewa akiwa kazini na kuwaachia huru watuhumiwa 13 na yeye mwenyewe kukimbia.
View attachment 3191272
Watu hao walikuwa wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi, ujambazi na mashambulizi.

Msemaji wa Polisi, Rae Hamoonga amesema Desemba 31, 2024 katika Kituo cha Polisi cha Cheelo jijini Lusaka, Inspekta Titus Phiri aliyekuwa amelewa, alichukua kwa nguvu funguo za vyumba husika kutoka kwa askari mwingine.

Kisha, inspekta huyo aliwafungulia watuhumiwa huku akiwaambia, "mpo huru kwenda kuupokea mwaka mpya".

Kati ya watuhumiwa 15, waliotoroka ni 13 na msako wa kuwatafuta unaendelea.

==

A police officer in Zambia has been arrested for allegedly releasing over a dozen prisoners so they could celebrate New Year’s Eve.

Detective Inspector Titus Phiri “forcibly seized cell keys” on Tuesday morning whilst “in a state of intoxication,” Zambia’s Police Service said in a press release on Wednesday.

“Subsequently, (Phiri) unlocked both the male and female cells and instructed the suspects to leave, stating they were free to cross over into the New Year,” the police statement said.

A manhunt has been launched for 13 detainees who remain at large, according to the police statement. Some had been facing allegations of assault and theft among other crimes, it said.

“The Zambia Police Service reiterates its commitment to upholding law and order and assures the public that decisive action will be taken against any officer found to be abusing their authority or acting contrary to the law,” it added
"mpo huru kwenda kuupokea mwaka mpya".- Mamlaka matamu aisee.
Very interesting story.

Wamsamehe tu huyo Askari Polisi
 
Hii nayo kali...!
TBT: Mwaka 1979 wakati vita ya Kagera imepamba moto, Mkuu wa Gereza fulani kule Bukoba aliwafungulia wafungwa ili kila mmoja ajiokoe nafsi yake!
Hiyo inaruhusiwa kabisa kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa kuhusu Haki za Binadamu na Sheria za kuhusu masuala ya Usalama wa Watu waliopo vizuizini.
Huyo Mkuu wa Gereza kwa hakika ali-qualify kupewa Cheo hicho cha Ukuu wa Gereza. Alikuwa anajuwa Wajibu wake pamoja na Haki zake kuhusiana na masuala ya Watu waliowekwa vizuizini.
Kongole kwake.
 
Zambia na Kenya ndio nchi zinazoongoza kwa vituko zaidi Afrika.
 
Hizi pombe kwa kweli ni janga jingine,sijui afande anatoa utetezi gani katika hili.Ni parenta administration kwa disciplinary authority ndiyo iliyobaki akiungama mbele yake.
 
Back
Top Bottom