Mkuu,kwanza pole sana!
Hapa nilipo nina modem 3,zantel nilinunua ya kwanza kabisa,sasatel na vodacom!
Naona atleast vodacom wako fair kiasi fulani,...
1.kwa vodacom
Kwa mimi natumia package ya limitless,ambayo unaweka elf30 then unapewa kwa mda wa mwezi mzima!
Ukae online 24hours shauri zako bora tu mwezi ukiisha package yako inakuwa imeisha!
Dis-advantege:speed yake inakuwa ndogo sana!
Au
Unaweza nunua package ya elfu10,limitless lakini kwa mda wa week moja,zote hizi disadvantege zao ni kwamba sometimes zinakuwa na speed ndogo ila kwa matumizi kama uliyo sema itakusaidia!
2.zantel
Package zao za elf10 wanatoa MB250 ambazo inabidi utumie kwa mwezi,...kilicho sababisha niitose zantel ni kama kilicho kukuta wewe,
Umenunua package ya elf10,ukapewa MB250 na ukazimaliza,..na zantel ukimaliza package yao hata kama uliweka leo kupewa package ingine ni hadi mwezi uishe,...so kila unapo jaza hela hupewi package ila unatumia hela yako kavu kavu na inapukutika kama majani!
3.sasatel,
hata sitaki kuisemea,kwa matumizi yako chukua voda itakusaidia,ingawa uwe makini modem za voda za sasa nyingi hazikubali kufanya kazi kwenye linux (hasa zile za elf49)