Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Naomba msaada kutoka mtu anayejua vizuri historia ya Zanzibar. Abdulrazak Gurnah aliyeshinda Tuzo la Nobel la Fasihi alizaliwa 1948 akaondoka kwenda Uingereza alipokuwa na umri wa miaka 18. Nimesoma mara kwa mara alipaswa kukimbia; magazeti mengi yanaandika kwamba alipaswa kuwa mkimbizi kwa sababu ya mateso ya wananchi Waarabu wa Unguja wakati wa mapinduzi. Nadhani wengi wanaojua historia hii kidogo wamshasikia kwamba wakati ule watu maelfu waliuawa hovyo kwa sababu walihesabiwa kuwa "Waarabu", na Gurnah alizaliwa katika familia iliyotazamiwa kuwa "Waarabu". (haongei Kiarabu bali Kiswahili, mababu walitoka Yemen).
Swali langu ni: Kama aliondoka akiwa na umwi wa 18, basi hiyo ilitokea mwaka 1966. Mimi nilifikiri hadi sasa kwamba mauaji na mateso makali ya "Waarabu" wa Unguja yalikwisha tayari baada ya miezi kadhaa kwenye mwaka 1964.
Hapa naomba msaada kama tunaye anayejua: je kulikuwa na matatizo tena mnamno 1966 yaliyoweza kumtisha kijana aliyeitwa "Mwarabu"?
Au je inawezakana alikataliwa kuingia katika A-level au chuoni kutokana na ukoo wake?
Nimeshangaa kwamba magazeti kote duniani yaliandika habari hizo bila kutafuta ufafanuzi kuhusu sababu kamili ya kukimbia kwake.