Tuwe na mtazamo chanya, uhuni unaofanywa na NEC,polisi na vyombo vingine wakati wa uchaguzi unawezekana kwa vile sisiem ndio mabosi wao,hivyo hatua ya maalim ni ataweza kupambana na wale vibaraka wa sisiem na kuweka watu makini kwa maslahi ya taifa,wanaoweza kuwasikiliza wananchi na kujali maslahi yao hasa pale yanapokuja maswala muhimu kama haya ya kuwachagua viongozi.Bara nasi tunatakiwa tufanye hivi kupigana nao hawa jamaa ukiwa nje ni kazi kweli kweli,embu angalia polisi wamejaa kila mahali wananchi wanapojaribu kudai haki ya kura zao na wanawapa kibano cha kweli kweli lakini inapokuja swala la usalama wakati ambao si wa uchaguzi utaambiwa kuna upungufu wa polisi,je!kuna aina mbili ya hao polisi(yaani kikosi cha polisi-kitengo cha kuwachakachua raia wadai hai na polisi doria ya kawaida),au wanawakodi mahali.