Leo Rais Mteule wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi anaapishwa kuyatwaa Rasmi madaraka ya kuingoza Zanzibar akimrithi Dr. Ali Mohamed Shein. Kwa sasa tayari wananchi na viongozi wameshawasili ikiwemo marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Kikwete.
=======
3:35 Asubuhi: Amewasili mkuu wa majeshi Tanzania, Venance Mabeyo. Pia amewasili Balozi Seif Ali Iddi, makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar.
3:47 Asubuhi: Amewasili waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa. Pia amewasili makamu wa Rais Muungano, Mama Samia Suluhu.
4:03 Asubuhi: Amewasili Dkt. Hussein Mwinyi na yanafanyika maandamano kuelekea jukwaa la kiapo yanayoongozwa na Jaji mkuu wa Zanzibar.
KIAPO(4:50 Asubuhi)
Jaji mkuu anasoma kifungu kinachomlazimu Rais mteule kula kiapo kabla ya kuchukua madaraka ya Rais kuiongoza Zanzibar. Baada ya hapo Dkt. Mwinyi anasoma kiapo na kuwa Rais wa awamu ya nane wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.
Dkt. Mwinyi: Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia Afya na kunirudhuku dhima hii kubwa iliyo mbele yangu ya kuwaongoza na kuwatumikia wananchi wenzangu wa #Zanzibar
Dkt. Mwinyi: Natambua wajibu unaoambatana na dhima hii ni kuwaongoza Wazanzibari kwa misingi ya haki, uadilifu na usawa
Dkt. Hussein Mwinyi: Kujitokeza kwenu kwa wingi kupiga kura ni kielelezo cha kukomaa kisiasa na kidemokrasia na kutambua kuwa Uchaguzi ndiyo njia sahihi ya kupata Viongozi wa nchi

Naipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa kukamilisha majukumu yake ya Kikatiba na Kisheria
Dkt. Mwinyi: Natambua wajibu unaoambatana na dhima hii ni kuwaongoza Wazanzibari kwa misingi ya haki, uadilifu na usawa
Kama nilivyozungumza wakati wa kupokea matokeo leo naomba nirudie, lengo letu ni kuijenga #Zanzibar. Zanzibar mpya inajengwa na sisi bila kujali tofauti zetu
Dkt. Hussein Mwinyi: Kujitokeza kwenu kwa wingi kupiga kura ni kielelezo cha kukomaa kisiasa na kidemokrasia na kutambua kuwa Uchaguzi ndiyo njia sahihi ya kupata Viongozi wa nchi
Rais Magufuli ameniagiza nifikishe salamu zake za pongezi kwa kufanikisha uchaguzi kwa usalama