Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,606
- 6,672
ACT-Wazalendo wataka uchunguzi ufanyike.
Ndugu Ali Bakari Ali amekutwa na Umauti Usiku wa kuamkia jana tarehe 29/03/2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja, kutokana na Majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa, kupigwa na kutupwa na watu wanaosaidikiwa kuwa ni Majambazi.
Mazingira ya kifo cha Ndugu Ali Bakar ni muendelezo wa vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikitokea katika Mji wa Zanzibar na viunga vyake. Kama tulivyowahi kusema hapo siku za nyuma kwamba vitendo vya uhalifu wa kikatili vinavyotokea Zanzibar ni wa aina na mbinu mpya za kihalifu ambao haujazoeleka Zanzibar.
Kuendelea kwa vitendo hivyo kunaashiria uwepo wa vikundi vya kihalifu ambavyo vinajiimarisha kila siku bila Jeshi la Polisi kuonesha uwezo wa kuvidhibiti kwa kukinga au kufanya upelelezi unaopelekea wahusika kutiwa hatiani.
Kwa sababu tulizoeleza hapo juu, Chama Cha ACT Wazalendo, tumepokea taarifa hii kwa uzito wake, na tunalitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha wanawakamata wahusika wote wa tukio hili la kinyama la kukatisha uhai wa mtu na kuwafikisha wahalifu hao katika vyombo vya sheria.
Kutokana na matokeo ya uhalifu ya kutekwa, kupigwa na kuumizwa raia wasio na hatia na makundi ya
kihalifu yaliyoripotiwa hivi karibuni, yanatia mashaka na hali ya wasisawasi kwa usalama wa watu na mali
zao. Matokeo haya hayaoneshi taaswira njema kwa nchi na yanatia kila aina ya wasiwasi na mashaka kwa Wananchi wa Zanzibar. Hivyo basi Chama chetu tunalitaka jeshi la Polisi na Serikali kufanya yafuatayo:
1. Jeshi la Polisi kuimarisha kitengo chake cha ufuatiliaji wa matokeo kihalifu: Matokeo kama haya yaliyoripotiwa hivi karibuni yote yanaonesha Jeshi la Polisi kutokuwa na taarifa za Kientelijensia na badala yake yanawakuta matokeo haya kama ajali na kugeuka kuwa chombo cha dharura cha kuokoa kuliko chombo cha kuzuia matokeo ya uhalifu na ulinzi wa raia.
2. Tunalitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa kwa Umma baada ya Uchunguzi na kuwakamata wahalifu na Taarifa walizochukua.
3. Tunalitaka Jeshi la Polisi, kutoa ushauri wa kipolisi kwa raia (Police Advisory) juu ya aina za uhalifu uliopo na namna ya kuchukua hatua za kukinga uhalifu huo.
4. Tunaitaka Serikali iyachukulie matokeo haya yanayoripotiwa kwa uzito wake kwa kuimarisha vitengo vyote vya ulinzi ili kuweka ulinzi katika maeneo yote ya Zanzibar hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Skukuu ya Pasaka.
Chama cha ACT Wazalendo, tunalitaka jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi, katika maeneo yote ya Zanzibar kutokana na matukio ya kihalifu na kinyama yanayoendelea kufanyika na kuripotiwa hivi karibuni katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
Imetolewa na:
Actrimariy Salim A. Bimani,
Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma,
Chama cha ACT-Wazalendo
30/03/2024
Chama Cha ACT Wazalendo, Tunalitaka Jeshi la Polisi Kuhakikisha, Linawakamata na Kuwafikisha Katika Vyombo Vya Sheria, Wote Waliohusika na Kifo Cha Katibu wa ACT Wazalendo, Jimbo la Chaani, Ndugu ALI BAKARI ALI
Chama cha ACT Wazalendo, tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa kitendo cha kutekwa, kushambuliwa na kutupwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kupelekea umauti kwa katibu wa Chama chetu wa Jimbo la Chaani Ndugu, ALI BAKARI ALI