Zanzibar kujiunga OIC kivyake vyake

Mimi nafikiri madai ya zanzibar ni mwendelezo ule ule wa kutaka kutambulika kimataifa. Kwa wanaosema kuwa lazima katiba ya Tanzania ibadilishwe ndipo OIC wairuhusu Zanzibar ijiunge wasisahau kuwa nchi hizo zinasubiri kwa hamu sana kumeguka kwa Zanzibar toka kwenye muungano au ndio wanaweza wakaishawishi zaidi ili iondoke kwenye muungano. Kwani Kosovo ambayo katika historia haijawahi kuwa nchi ilipojitenga si ilitambiliwa na baadhi za nchi haraka haraka pamoja na kwamba Serbia imepinga jambo hilo? Sembuse Zanzibar ambayo hapo nyuma ilikuwa na balozi katika nchi mbalimbali? Wao wameshaamua na tukiendelea kuwakataza yataibuka mengine mpaka nia yao ya kuondoka kwenye muungano itimie.

Si tusibiri, ni suala la muda tu
 
Mkuu Mwiba, vipi hili jambo, ni miaka 10 sasa, na itapita 10 mingine.
Sasa jambo dogo tuu kama hili limeshindikana, then jambo kubwa la Muungano mtaliweza?.
P
 
Zanzibar haiwes kuamua kufanya inachotaka kufanya, zanzibar ni moja wapo ya muungano, hvyo mpaka wajitoe kweny muungano ndipo wataweza jiunga, na kujitoa kwa muungano ni jammbo jingine...tulishaunganishwa na mwalimu...sasahv yeye hayupo....mpka afufuke labda ndo zanzibar itajitenga...otherwise...tuendelee kula biriani...
 
Katiba inasema watu wana dini...wataabud popote...ila serikali haina dini.....OIC hapo haina chake.......wanataka kutuchanganya tu..na hilo pepo alishalikataa Jakaya......licha ya kuwa upande ule.......
 
Acha kuzungumza Pumba, Gabon, Uganda, Cameroon, Benin wao ni nchi za dini gani? mbona wamo?
Brazil, South Africa, Serbia wote walifanya attemp zao kujiunga nawao ni nchi ya dini gani?
Punguza chuki mkuu
 
Ukitaka uwaone watanganyika wakija juu awe chadema, ACT, awe CCM awe CUF ya msaliti lipumbavu basi andika juu ya suala la muungano au OIC. Mimi binafsi namuunga mkono mheshimiwa Hamza juu ya jambo hili. Hofu yangu ni kuwa viongozi wa juu wa SMZ watampinga Hamza na watasema hayo yalikuwa ni mawazo yake kama Hamza na hayawakilishi mawazo ya serikali.
 
Acha kuzungumza Pumba, Gabon, Uganda, Cameroon, Benin wao ni nchi za dini gani? mbona wamo?
Brazil, South Africa, Serbia wote walifanya attemp zao kujiunga nawao ni nchi ya dini gani?
Punguza chuki mkuu

wanaobisha Znz kujiunga na OIC ni myopic. si kwamba watanganyika hawajui kuwa OIC si jumuiya ya kimataifa yenye focus ya kidini, wanajua ila wanaendeleza ile dhana ya znz isiwe na maamuzi yake na ibaki ktk duara la mtawala na mtawaliwa. Wako wengine wanachuki dhidi ya znz wanafikiri OIC ni udini na ugaidi.
 
Mkuu Mwiba, vipi hili jambo, ni miaka 10 sasa, na itapita 10 mingine.
Sasa jambo dogo tuu kama hili limeshindikana, then jambo kubwa la Muungano mtaliweza?.
P

Walijiungs mwaka 1992, je ni sheria ipi iliwaondoa?
 
Kuna athari gani kwa Tanganyika kuiachia zanzibar ikajiunga na OIC? Tujadili hapa kwanza kuliko kuja na vuvuzela zisizoisha eti znz eti znz haiwezi kujiunga na jumuiya za kimataifa kwa kuwa sio nchi bali ni sehemu ya JMT.
 
Mkuu Mwiba, vipi hili jambo, ni miaka 10 sasa, na itapita 10 mingine.
Sasa jambo dogo tuu kama hili limeshindikana, then jambo kubwa la Muungano mtaliweza?.
P

Philosophy and practice ya ukoloni dhidi ya znz bado iko hai. Karume amefanya makosa sana na wala hatutamsamehe kuingiza znz ktk ukoloni wa tanganyika. Paskali upo? kwa heri ukoloni kwa heri uhuru. - Dr Gharith Ghassan
 
Kuna athari gani kwa Tanganyika kuiachia zanzibar ikajiunga na OIC? Tujadili hapa kwanza kuliko kuja na vuvuzela zisizoisha eti znz eti znz haiwezi kujiunga na jumuiya za kimataifa kwa kuwa sio nchi bali ni sehemu ya JMT.

kumbuka Zanzibar jibu ililopewa na CAF kwamba maana nchi inatoka UN na kule Zanzibar haihesabiki kama nchi.
 
Basi si mtuache tupumue . Nini tatizo? Wallahi nyie tukiwa huru nje ya muungano njooni znz baada ya miaka 10 mtaona mabadiliko makubwa sana ya kijamii na kiuchumi. Tutakuacheni kwa mbali sana.
 
Philosophy and practice ya ukoloni dhidi ya znz bado iko hai. Karume amefanya makosa sana na wala hatutamsamehe kuingiza znz ktk ukoloni wa tanganyika. Paskali upo? kwa heri ukoloni kwa heri uhuru. - Dr Gharith Ghassan
Mkuu Kibwengomfupi, poleni. Wote wanaomlaumu Karume kwa Muungano na kuita ukoloni wa Tanganyika mnajichumia tuu dhambi bure. Andiko la Kwaheri Kwaheri limejaa urongo mwingi. Urongo mkubwa kuliko ni eti yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yalipangwa bara na watekelezaji ni Wamakonde wakata mikonge kutoka Tanga!.

Kuna Wanzanzibari wengi hawakupata kumjua vizuri Karume alikuwa mtu wa aina gani, kiukweli kabisa Muungano umewasaidia sana na Nyerere amewasaidia sana kwa Karume, bila Muungano, kuna wengi wenu saa hizi ingekuwa ni history, sii wengi mnajua Karume alikuwa anawafanya nini, kama sii Nyerere kuna watu hata kaburi msinge liona, ni vile tuu hamjui Nyerere alisaidia nini. Muwe watu wa shukrani.

P
 
trekta 50? trion 2:4 unaifahamu ? bilion 1.5 inanunua hayo 50 haina haja ya kujiunga
 
Mkuu pasikali kwanini tuendeleze kuwalazimisha wazanzibar juuu ya muungano. ? ikiwa kwao ndo una manufaa.

Kwa ilipofikia zanzibar kama si Maslahi ya watanganyika siioni hoja yenye mashiko kuwalazimisha juu ya huu muungano.
USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO
 
Yaani trekta 50 ndiyo iwe sababu? Au kuna hoja nyingine ambayo msemaje ameshindwa kuitaja na anajificha nyuma ya kisingizio cha trekta 50.
 
Hakuna mtu analazimisha Muungano, bali Muungano wetu adhimu ni udungu wa damu baina yetu. Kwa Wazanzibari asili na halisi wanapenda Muungano, na asili ya halisi ya Zanzibar ni sehemu ya Azania ikamegeka miaka milioni nyingi nyuma.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…