Zanzibar 2020 Zanzibar: Maalim Seif atangaza kupiga kura leo badala ya kesho Oktoba 28

Zanzibar 2020 Zanzibar: Maalim Seif atangaza kupiga kura leo badala ya kesho Oktoba 28

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema, atapiga kura siku ya kwanza Jumanne tarehe 27 Oktoba badala ya siku ya uchaguzi Oktoba 2020.

Maalim Seif amesema hayo leo Jumatatu tarehe 26 Oktoba 2020 wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu kura ya mapema inayofanyika leo kwa watumishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na watumishi watakaosimamia siku ya uchaguzi mkuu.

Mwanasiasa huyo amesema, atapiga kura katika Kituo cha Garagara na atawasili kituoni hapo saa 2:30 asubuhi. "Mimi napiga kura katika Kituo cha Garagara na nategemea saa 2:30 asubuhi kwenda kupiga kura. Ni haki yangu,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif amesema, uamuzi wakupiga kura ya mapema unatokana na ZEC kushindwa kutoa takwimu za wapiga kura ya mapema.

“Kwa kuwa ZEC imeshindwa kutoa takwimu za Wapiga kura ya mapema na pia, kushindwa kuweka wazi majina ya wapigakura hadi sasa, niwatake wananchi wote kujitokeza kwa wingi Jumanne katika vituo vyote vya kupigia kura. Wananchi wote wajitokeze kwa amani, bila vurugu na kudai haki ya kupiga kura kwa amani,” amesema Maalim Seif.

Aidha, Maalim Seif amewataka wananchi watakaoshindwa kupiga kura leo wajitokeze kutimiza wajibu wao huo Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020.

“Pamoja na kuwepo kwa masuala mengi yasiyo na majibu mpaka sasa kutoka kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, hali inayothibitisha mashaka yetu kuwa ZEC haipo kuendesha uchaguzi huru, wa haki na wa wazi.”

“Wazanzibari wanapaswa kufahamu ni umoja wetu na mshikamano wetu ndio utakaoleta mabadiliko ya kweli nchini,” amesema Maalim Seif.

MwanahalisiOnline
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku).

Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Dogo ushawahi hata piga kura?..weka jazba wenzio wakilianzisha wanakimbilia ubelgiji...we utanyea debe
 
Dogo ushawahi hata piga kura?..weka jazba wenzio wakilianzisha wanakimbilia ubelgiji...we utanyea debe
Uzuri mnaowategemea hamjawaongezea mishahara tegemeeni kugeukwa sijui mtategemea nn tena
 
Two wrongs doesn't make one right.
Sababu tu zec hawajatoa majina na idadi ndio uanzishe ujinga huu maalim seif? Nafikiri ingetosha kuishauri tume hao wapiga kura wa tarehe 27, waje na vitambulisho vya kazi ili kujirizisha kuwa ni kweli kundi maalum la wasimamizi wa uchaguzi, km askari na wafanyakazi wa tume. Hawa nao wana haki ya kupiga kura. Tatizo lipo wapi? mawakala wenu si wapo jamani?
Ebu acheni nchi isonge jamani sio kila kitu kuleta ubishi tu.
 
CCM wanafanya mambo ya ajabu sana Zanzibar. Yaani ZEC hawafanyi chochote bila kupokea maelekezo na maagizo kutokea Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom