Zanzibar Mix

MadameX

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2009
Posts
7,792
Reaction score
3,856
1 kg Viazi mviringo/ulaya
1/2 kikombe unga wa ngano
1 kijiko bizari(rangi ya mchuzi)
4 malimau/ndimu au upendavyo
chumvi kiasi
6 ltrs maji...yakutosha kuivisha

Namna ya kupika

1)Chemsha viazi kwenye maji 4 ltrs na maganda yake mpaka ziwive lakini zisivurugike,zikiiva zimwage maji ziweke pembeni.


2) Tia maji 2 ltrs ktk sufuria weka jikoni, koroga unga wako wa ngano ktk bakuli utie maji na bizari uchanganye uwe hauna madonge na uzito uwe kama wa mkate wa maji uzidi kidogo tu.


3) Maji yakipata moto utie unga wako huku unakoroga usiachie mkono mpaka uone umeshikana kama uji, punguza moto tia chumvi, kamua malimau au ndimu ktk kibakuli towa kokwa tia huo ukali ktk urojo, onja kiasi chako raha ya urojo uwe mkali kidogo,

3) Menya viazi vyako uvikate vipande saizi sio vikubwa, vitumbukize kwenye urojo acha vichemke kama dakika 5 hivi, epua, tia kwenye bakuli.


4) Hapo kama mpenzi wa bajia, crips, chips za mhogo, chatne unaziweka na kukoroga na tayari kwa kuliwa
 
nilijua tu madam b ni mtu wa pwani.maneno yako tu malimau,bizari ni ya ki znz hasa.nilivyokuwa mjamzito nilikula sana hizi mix.sasa hivi hata unipe bure sizitaki
 
Pale upanga ndo.pa kwenda kudusa hii makitu na zile.bajia wanachanganyia na tumishkaki tuduchuu. Zenj mambo yote kwenye ile mishkaki ya samaki. Nami sio mpenzi sana wa urojo ila walau sasa nna idea wanapikaje. Asante mamito.
 
1)Chemsha viazi na maganda yake

2) Tia maji ktk sufuria weka jikoni,

koroga unga wako wa ngano ktk bakuli utie maji
3) Maji yakipata moto utie

3) Menya viazi vyako uvikate vipande saizi

Tia maji katika sufuria... maji ndoo ngapi?

Ukate vipande saizi... vipande saizi ndio saizi gani?

Maji yakipata moto utie unga... moto wa temperature ngapi?

Recipe za kiholela holela utadhani unaandaa chakula cha nyoka!?

Tunataka Tanganyika mix, hatutaki Zanzibar mix wala Zanzibar karafuu wala anything Zanzibar!
 
nilijua tu madam b ni mtu wa pwani.maneno yako tu malimau,bizari ni ya ki znz hasa.nilivyokuwa mjamzito nilikula sana hizi mix.sasa hivi hata unipe bure sizitaki

Wewe kwenu wapi? Mwembeladu au Bububu?:becky:
 

Asante kwa marekebisho...kuna vitu ni common sense kama huna common sense ya jikoni its difficult to explain. Kama ni mwanaume nitafahamu kama ni mwanamke mmmh hebu ongeza juhudi.

Jamani sio cake hii wala biscuit, vyakula vyetu vyingi vya uswahili ni kujua mahitaji na jinsi ya kupika. Size inatokana na idadi ya walaji
 
Na viazi vitamu vikichemshwa kwa maharage na kuungwa mawese acha kabisa! Au Kisati/mnyemwe asubuhiii
 
nakumbuka nilikuwa mpenzi wa urojo wakati nasoma pale muhimbili!
 

mchaga na mapishi wapi?kachemshe milopoo ya damu na ndizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…