A
Anonymous
Guest
Inawezekana hili ni jambo lisilosemwa ila ukweli huu hakuna mwenye nguvu ya kuupinga.
Nalieleza hili kwa kuwasaidia watoto wakimaskini ambao hawana watu wakuwapigania(connection), na kuinusuru Zanzibar isitumbukie shimoni ambako kutamlazimu mwenye sifa kukosa kazi na asie na sifa apate kwasababu tu yeye ni CCM au ni jamaa wa kizito serikalini.
Tume ya Utumishi Serikalini imekuwa ikifanya hatua zifuatazo wakati wa kuajiri.
1. Matangazo: Hapa tume huwatangazia watu nafasi wanazohitaji na kuwaelekeza watu kutuma maombi kupitia tovuti ya Zanajira.
2. Usaili: hapa usaili ni aina mbili,
a. Usaili wa maandishi ambapo huwataka watu waliotuma maombi kufika kituo husika na kufanya usaili wa maandishi hapa sijui kunatumika vigezo gani lakini huenda baadhi ya wasiliwa wasiendelee hatua ya pili ya usaili.
b. Usaili wa ana kwa ana, ambao huhusisha ukaguzi yakinifu wa vyeti pamoja na mahojiano ya ana kwa ana baina ya tume na waajiriwa.
Baada ya hatua hizi sasa wasailiwa wanatakiwa kusubiri simu ya kuitwa kujaza mkataba na hatimae kuanza kazi.
Hapa kwenye simu ndipo ilipo shida.
Kwasababu hapa atapigiwa simu mtu ata ambae kwenye usaili hakuwepo.
Atapigiwa simu mtu ambae hata sio kipaumbele cha Wizara.
Atapigiwa simu mtu ambae ana mtu wake serikalini.
Atapigiwa simu mtu ambae kahonga pesa ili kupata nafasi.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi tutakosa watumishi wenye weledi na uzalendo katika kazi zao.
Suluhisho, Watakaokubalika kwenye usaili kwa taratibu na malengo ya wizara husika basi majina yao yawekwe wazi na yaonekane na kila mtu.
N:B
a. Naomba hili lifike kama lilivyo
b. Na ikiwa yupo atakaekanisha basi nitaweka wazi maafisa wa serikali wanaofanya hii biashara.