Zanzibar na uchumi unao wapa maisha ya umasikini wananchi wake.

Zanzibar na uchumi unao wapa maisha ya umasikini wananchi wake.

wrong turn

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
438
Reaction score
170
Kwa muda mrefu sasa Zanzibar imekuwa katika hali mbaya ya kiuchumi huku wanachi wake wakihangaika na kutapatapa katika kuokoa maisha yao kwahali yoyote ile.

Ukifuatilia historia, Zanzibar inaoneka ilikuwa ni nchi ya kibiashara Afrika Mashariki lakini inekuwa tofauti na sasa, Zanzibar inamaeneo mengi na yenye mvuto kibiashara lakini watendaji ndio vikwazo kwa maendeleo.
Mji wa Zanzibar nikitovu kikuu cha biashara kwa sasa lakini mji huo hauonekani kuwa katika hali ya kibiashara kwani hivi karibuni kulikuwa na hali ya mvutano kati ya wafanya biashara na serekali kwa kutaka kuligeuza eneo la darajani kuwa sehemu ya mustani wakati wafanya bishara wakita pawe eneo la biashara.

Sielewi serekali inmaana gani kwa wananchi wa Zanzibar na nchi za Afrika Mashariki, hadi sasa Zanzibar inategemea secta ya utalii, hakuna kilimo wala biashara ya nazi au karafuu inayo leta pato kubwa kama hapo awali alivyokuwa.

Hivi karibuni tumeona hatua nzuri katika secta ya usafiri wa majini kati ya Zanzibar na Dar es salaam kwa kujengwa kwa eneo la kusubiria boti, nihatua nzuri kwa compuni ya azam kwa kuekeza katika maeneo ya kijamii. Ujenzi wa jengo hilo liko katika hatua nzuri na yakuvutia na lina hadhi ya kinataifa.

Sijui ingalikuwa wapi Zanzibar kama ingekuwa na viongozi wabunifu na wenye kutaka maendeleo kwa wananchi wake, kiukwae viongazi wa Zanzibar wamechoka kuhudumia wananchi wake na kwavile watanzania hatuna utamaduni wa kujiondoa katika madaraka ndio chanzo kikubwa cha umasikini usio kwisha.
 
Back
Top Bottom