A
Anonymous
Guest
Ustadhi wa Madrasa mwenye umri wa miaka 70 anayeishi hapa mtaani kwetu, ana tuhuma za kumbaka binti wa Miaka 16 mara kadhaa hadi kumsababishia hasara, kinachouma zaidi ni kwa kuwa mtuhumiwa ni Askari wa zamani na Jeshi la Polisi hapa Zanzibar ni kama linamlinda.
Skendo hii ilipoibuka tukaanza kupewa vitisho kadhaa watu wa mtaani, baadaye kuna Waandishi wa Habari, walienda kumhoji mhusika lakini kilichofuata wakapata vitisho vikali.
Wakatangaza kuwa yeyote ambaye atakuwa na kiherehere watadili naye.
Ipo hivi, mwanzoni mwa Mwaka huu 2024, Mtoto (muathirika) alianza kugoma kwenda Madrasa, ndugu zake hawakuelewa tatizo ni nini, kumbe alikuwa ameshachoka kile alichokuwa anafanyiwa na Mwalimu huyo wa Madrasa.
The Chanzo walivyoripoti tukio hilo Januari 2024
Huyo Mwalimu wa Madrasa anafundisha Watoto kadhaa nyumbani kwake ambapo pia ni upande wa nyuma ya nyumba anayoishi na familia yake.
Alikuwa Kidato cha Kwanza na Januari 2024 alitakiwa kuingia Kidato cha Pili, alichokuja kutusimulia baadaye ni kuwa, kuna siku Mwalimu huyo alimtuma Binti mhusika kununua soda ya Sprite.
Mtuhumiwa
RB Namba
Hiyo ilikuwa siku ya kwanza mtoto huyo kufanyiwa ukatili, ilikuwa nyumbani kwa Mwalimu wakati huo familia yake haikuwepo.
Alipofika akamkabidhi Mwalimu, akaingia ndani, Mwalimu aliporejea akiwa na soda iliyopungua nusu, akampa Mtoto anywe.
Mtoto alisimulia kuwa anasema alipokunywa baada ya muda hakuelewa kilichoendelea, akaja kushtuka akiwa amelala huku ana maumivu makali sehemu za siri na akiwa amelowa damu.
Mtoto akasema kuwa aliendelea kufanyiwa hivyo mara tatu nyakati tofauti huku akimtisha kuwa akisema atamuua.
Baada ya muda tumbo likaanza kuwa kubwa, ndugu wakashtuka na kwenda kumfanyia vipimo katika Hospitali ya Mbuzini, ikabainika ana ujauzito.
Mtoto akamtaja Mwalimu wake wa Madrasa, wakaenda kufungua mashtaka katika Kituo cha Polisi Mwera, wakafungua mashtaka matatu ambayo ni kumbaka Mwanafunzi, kumpa ujauzito na kumtorosha akiwa chini ya uangalizi wa Wazazi wake.
Mtuhumiwa akakamatwa lakini baadaye wakamuachia kwa dhamana, walifanya hivyo licha ya Rais Mwinyi kusema mara kadhaa kuwa watuhumiwa wenye kesi ya ubakaji hawastaili dhamana.
Ndugu wakaenda hadi Ustawi wa Jamii, Polisi walipoulizwa wakadai mtuhumiwa ataendelea kuwa nje kwa kuwa wanasubiri muongozo wa vipimo vya DNA ambavyo vitafanyika mtoto atakapozaliwa.
Inamaanisha wakikuta kweli huyo mtuhumiwa ndiye mhusika watafanya nini?
Kinachoumiza zaidi ndugu wa mtoto wengi wao wana hali ya kipato cha chini, wametuma barua kwa viongozi wa juu lakini hawajui kama zimefika au la.
MAMA WA BINTI ANALIA TU
Tukio hilo limekuwa likimfanya mama mtoto awe analia tu, ni kama hayupo sawa Kisaikolojia.
Kibaya zaidi mtuhumiwa aliwahi kuwa na skendo siku za nyuma ya kumpa ujauzito mtoto wa ndugu yake ndio maana akafukuzwa kazi.
Mama mtu amekuwa akilia muda mwingi, akiona nguo za shule za mwanaye anaishia kuwa katika wakati mgumu, kinachomuumiza zaidi ni kwamba anaingia gharama kubwa kwa ajili ya mtoto wake, anachangishana na familia yake kwa ajili ya kumhudumia Mtoto.
WANAHABARI WANATISHWA
Wanahabari wakienda kuhoji wakitoka hapo hawatoi hiyo Habari kwa kuwa wanaogopa kutokana na vitisho, na sasa mtoto anakaribia kujifungua huku familia yake ikiwa haijui hatma ya kitakachofuata.
Naomba Serikali iwasaidie hawa wana Familia na haki itendeke, Mtuhumiwa sasa hivi tunaambiwa amekimbia Mji bada ya mkewe kuomba talaka kutokana na 'aibu' inayoendelea.
Pia soma - Matukio ya Ukatili wa Kijinsia yaripotiwa kuongezeka Visiwani Zanzibar