Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku

uswaa

Member
Joined
Mar 4, 2014
Posts
55
Reaction score
20
Nianze kwa kunukuu tangazo nililokuta Bagamoyo, nilipokwenda katika shughuli zangu za kutoa ushauri kuhusu maendelezo bora ya ardhi eneo la makurunge ili kunogesha mjadala katika makala yangu leo ubaoni.

Tangazo liliandikwa hivi: TAHADHARI! USIKUBALI KUNUNUA ARDHI/SHAMBA KATIKA ENEO LILILOKUWA SHAMBA LA RAZABA. SHAMBA HILI LINALOAMBAA KATIKA MAENEO YA MAKANI, MAKURUNGE, GAMA NA MTO WAMI NI SHAMBA LA SERIKALI NA TAYARI LIKO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUMILIKISHWA KWA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA ECOENERGY" Mwisho wa kunukuu.

Tangazo hilo liliwekwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo tarehe 21 Novemba 2011 na kuibua hoja zangu kubwa mbili.

Kwanza RAZABA ni nini na Serikali ni nani maana tangazo linasema shamba lililokuwa la Ranchi ya Watu wa Zanzibar (RAZABA) pia inataja shamba la Serikali na kwa nini matumizi yake yanabadilishwa.

Pili watu wasinunue ardhi katika eneo hilo kutoka kwa nani?

Kuna raia wanaishi humo? Kwa amri ya nani na waliingiaje humo?

Maaana halisi ya neno RAZABA ni Ranchi ya Zanzibar, Bagamoyo (Ranch of Zanzibar in Bagamoyo)

Kwa simulizi kutoka kwa watangulizi wetu eneo la RAZABA ilikuwa ni zawadi ya Mwalimu Nyerere kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na lina ukubwa wa zaidi ya hekta elfu ishirini na nane.

Mto Wami, reli ya Tanga, Barabara ya Bagamoyo Msata, mto ruvu na bahari ya hindi ndio mipaka halisi ya RAZABA.

Mmiliki wa RAZABA ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar! Kwa maana halisi, RAZABA ni eneo la Zanzibar ndani ya Tanganyika.

Hayati Mwalimu Nyerere alitoa eneo hilo ili kuwapa fursa Wazanzibari kumiliki mifugo yao wenyewe, na mifugo yote inayotoka maeneo ya Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma na kwingineko kwenda Zanzibar, ifikie RAZABA kabla ya kusafirishwa kwenda kutumiwa na wananchi wa Zanzibar.

Leo biashara ya ardhi kati ya RAZABA na ECOENEGY inafanywa na nani? Serikali ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar? Kwa manufaa ya nani? Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanganyika au Serikali ya muungano? Matumizi yaliyopangwa wakati wa kutenga eneo la RAZABA hivi sasa yamepitwa na wakati?

Wananchi wa Zanzibar hivi sasa wamesitisha ulaji wa nyama kutoka bara au wamepata mbadala? Lakini kwa kutumia akili ndogo kabisa, hivi mbadala wa nyama Zanzibar zaidi ya kuitegemea Tanganyika ni upi? Upo kweli? Kulikuwa na mantiki kubwa sana kuweka rachi katika eneo linalosemwa lilikuwa la RAZABA.

Kwanza kuna reli ambayo inarahisisha usafirishaji wa mifugo kutoka bara inapopatikana kwa wingi, kuna mito miwili inayofanya urahisi wa kupatikana kwa maji kwa ajili ya mifugo, barabara ni ya uhakika lakini kikubwa zaidi, Bahari ya Hindi inayounganisha Visiwa vya Zanzibar na Mji wa Bagamoyo.

Pia kwa mtazamo wa mbali tungejenga hata kiwanda cha kusindika nyama na samaki ili tutumie vyema bandari kubwa inayojengwa Bagamoyo kuuza nyama iliyosindikwa nje ya nchi. Leo tunapoiua RAZABA, mbadala wake ni nini?

Sina maana ya kupinga mradi au uwekezaji wa kilimo cha miwa kwa ajili ya nishati mimea (bio fuel) unaokuja kufanywa na ECOENERGY, lakini kwa ardhi yote tuliyonayo Tanzania tunashindwa kuwatafutia ECOENERGY eneo jingine ambalo halijawahi kupangiwa matumizi?
 
Serikali ya halmshauri ya mji wa bagamoyo imewataka wananchi wanao nunua ardhi katika halmshauri hiyo kuwa makini hasa katika eneo la RAZABA makurunge kutokana na eneo hilo kutengwa kwa ajili ya matumizi ya serikali tangu mwaka 1977 ambapo watu wengi wameuziwa bila kufuata taaratibu hivyo serikali haitahusika na utapeli huo kwa wote waliouziwa viwanja katika eneo hilo.
Aidha serikali imewasihii wananchi wote kununua ardhi kwa kushirikiana na serikali ya halmshauri husika....

Nunua ardhi na dalalimsomi kuepuka matapeli wa ardhi.

Taarifa kwa umma... Ndugu wateja wa DALALIMSOMI
Nipende kuwataarifu kuwa makini pindi mnunuapo maeneo au viwanja katika halmshauri ya bagamoyo kutokana na utapeli unao endelea.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA ARDHI/KIWANJA AU NYUMBA (ili ununue ardhi salama)

[emoji637]. Mshirikishe mpima ardhi (land surveyor), mpima ardhi anahitajika ili aweze kukufanyia ukaguzi wa eneo lako ili kutambua eneo husika limepangiwa kwa ajili ya matumizi gani katika ramani ya mipango miji (ambayo ni ramani inayoonyesha matumizi mbalimbali ya katika ardhi mf barabara, makazi,eneo la wazi n.k) mara nyingi ni kwa maeneo yasiyo pimwa au yaliyopimwa ila hayana hati miliki.

[emoji638]. Shirikisha majiran wa eneo unalotaka kununua, ili uweze kutambua muuzaji wa eneo ni halali au sio, na pia itakusaidia kujua kama eneo halina migogoro. (Fanya mahojiano na majiran bila muuzaji kujua)

[emoji639]. Hakiki umiliki wa eneo husika serikali ya mtaa au kama kiwanja kimepimwa basi unaweza kupata taarifa zake halmashauri husika.
Unaweza kufanya mwenyewe au kwa kumtumia mpima ardhi au mwanasheria.
[emoji640]. Tengenezeza mikataba ya mauziano ya ardhi (sale agreement) ambayo huandaliwa na kusimamiwa na mwanasheia

[emoji641]. Kamilisha malipo kwa njia sahihi ya kibenki(usilipe cash lipia bank)

NB; Usiamini maneno toka kwa uongozi wa mtaa kuhusiana na matumizi ya eneo maana ni ngumu kuwa mkweli na pia kujua matumizi ya eneo husika unahitaji taaluma kujua hilo hasa kwa ardhi ya mjini mfano eneo lolote la dar esal salaam kwasababu dar es salaam ndo mkoa pekee Tanzania usio kuwa na kijiji kwa mujibu wa wizara ya ardhi.

By
@surveyormunkondya
@surveyormunkondya
@surveyormunkondya (Mpima ardhi)

FIKA OFISINI SINZA LEGHO OPPOSITE YA KIWANDA CHA TANICA
MAWASILIANO
Simu&whatsapp
0765532858
0673540985

IMG-20191008-WA0002.jpeg
 
Bagamoyo hakuna halmashauri ya mji ni halmashauri ya wilaya

Bagamoyo kuna Halmashauri tatu; Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo na Halmashauri ya Mji wa Chalinze.
 
Dah hii habari watu wengi walipuuza sasa nidhahiri
 
Mwamba aliandika ishu ya msingi sana, ila alipotezewa na wana JF
 
Duuuh report hii ilishiba miaka hio. RAZABA OYEE.
Kumbe waliazimwa tu tangu 1977 waweke ng'ombe, mbuzi, nguruwe, punda na kuku.
Sasa Makhanith i washaanza kusema lilikuwa la Mjerumani akampa Sultani. Uongo wa kubana pua kishog a kama kawaida
 
Nianze kwa kunukuu tangazo nililokuta Bagamoyo, nilipokwenda katika shughuli zangu za kutoa ushauri kuhusu maendelezo bora ya ardhi eneo la makurunge ili kunogesha mjadala katika makala yangu leo ubaoni.

Tangazo liliandikwa hivi: TAHADHARI! USIKUBALI KUNUNUA ARDHI/SHAMBA KATIKA ENEO LILILOKUWA SHAMBA LA RAZABA. SHAMBA HILI LINALOAMBAA KATIKA MAENEO YA MAKANI, MAKURUNGE, GAMA NA MTO WAMI NI SHAMBA LA SERIKALI NA TAYARI LIKO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUMILIKISHWA KWA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA ECOENERGY" Mwisho wa kunukuu.

Tangazo hilo liliwekwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo tarehe 21 Novemba 2011 na kuibua hoja zangu kubwa mbili.

Kwanza RAZABA ni nini na Serikali ni nani maana tangazo linasema shamba lililokuwa la Ranchi ya Watu wa Zanzibar (RAZABA) pia inataja shamba la Serikali na kwa nini matumizi yake yanabadilishwa.

Pili watu wasinunue ardhi katika eneo hilo kutoka kwa nani?

Kuna raia wanaishi humo? Kwa amri ya nani na waliingiaje humo?

Maaana halisi ya neno RAZABA ni Ranchi ya Zanzibar, Bagamoyo (Ranch of Zanzibar in Bagamoyo)

Kwa simulizi kutoka kwa watangulizi wetu eneo la RAZABA ilikuwa ni zawadi ya Mwalimu Nyerere kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na lina ukubwa wa zaidi ya hekta elfu ishirini na nane.

Mto Wami, reli ya Tanga, Barabara ya Bagamoyo Msata, mto ruvu na bahari ya hindi ndio mipaka halisi ya RAZABA.

Mmiliki wa RAZABA ni Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar! Kwa maana halisi, RAZABA ni eneo la Zanzibar ndani ya Tanganyika.

Hayati Mwalimu Nyerere alitoa eneo hilo ili kuwapa fursa Wazanzibari kumiliki mifugo yao wenyewe, na mifugo yote inayotoka maeneo ya Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma na kwingineko kwenda Zanzibar, ifikie RAZABA kabla ya kusafirishwa kwenda kutumiwa na wananchi wa Zanzibar.

Leo biashara ya ardhi kati ya RAZABA na ECOENEGY inafanywa na nani? Serikali ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar? Kwa manufaa ya nani? Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanganyika au Serikali ya muungano? Matumizi yaliyopangwa wakati wa kutenga eneo la RAZABA hivi sasa yamepitwa na wakati?

Wananchi wa Zanzibar hivi sasa wamesitisha ulaji wa nyama kutoka bara au wamepata mbadala? Lakini kwa kutumia akili ndogo kabisa, hivi mbadala
wa nyama Zanzibar zaidi ya kuitegemea Tanganyika ni upi? Upo kweli? Kulikuwa na mantiki kubwa sana kuweka rachi katika eneo linalosemwa lilikuwa la
RAZABA.

Kwanza kuna reli ambayo inarahisisha usafirishaji wa mifugo kutoka bara inapopatikana kwa wingi, kuna mito miwili inayofanya urahisi wa kupatika
kwa maji kwa ajili ya mifugo, barabara ni ya uhakika lakini kikubwa zaidi, Bahari ya Hindi inayounganisha Visiwa vya Zanzibar na Mji wa Bagamoyo.

Pia kwa mtazamo wa mbali tungejenga hata kiwanda cha kusindika nyama na samaki ili tutumie vyema bandari kubwa inayojengwa Bagamoyo kuuza nyama iliyosindikwa nje ya nchi. Leo tunapoiua RAZABA, mbadala wake ni nini?

Sina maana ya kupinga mradi au uwekezaji wa kilimo cha miwa kwa ajili ya nishati mimea (bio fuel) unaokuja kufanywa na ECOENERGY, lakini kwa
ardhi yote tuliyonayo Tanzania tunashindwa kuwatafutia ECOENERGY eneo jingine ambalo halijawahi kupangiwa matumizi?
Kwanza tukubali bila uya wasiwasi kuwa Hiyo sehemu inamilikiwa na SMZ.
Mfalme wa SMZ aliyepo amepata mfadhili kwa manufaa yake na kutaka kuwapa wawo.
Ndio hili Tangazo limetoka.
 
Asante sana kwa bandiko hili. Nimepata mwanga.
P
 
Ok investigative journalist njoo sasa umalizie hii mada, nani anafanya huo uwekezaji wa ECOENERGY? Au wazenji wamebadili matumizi ya ardhi waliyoazimwa bila idhini ya bunge la JMT, au ardhi imerudishwa kwa watanganyika ( hii katu haiwezekani ukizingatia madam ni wa huko), au mtoto wa mjini ameamua kuipora iwe yake binafsi ( ntacheka sana), au wameirudisha kimyakimya ili wavunje muungano kimyakimya ( kwa mujibu wa ndumilakuwili wa SANI ukiona watu wanakukimbiza kimyakimya wanataka kukuua!!!)
 
Wazanzibari wana uzalendo wa kutetea sana nchi Yao, JMT haina mwenyewe wa kutetea Wala kuisemea, hali ni mbaya zaidi Sasa ambapo boss wa JMT ni mzenji, kwa hio kujadili maswala ya muungano mzenji wa bara anakutana na mzenji wa visiwani kujadili hatma ya JMT, na watu wanaona ni sawa tu

Nawaza hio Katiba watu wanayoidai itakuwa vituko vya karne, wazenji ndio wenye karata ya turufu juu ya aina gani ya muungano wanautaka.

Kwa sababu CCM ndio itakuwa na wajumbe wengi, ikifuatiwa na taasisi za serikali Kama vyuo, CCM bara watasimamia msimamo wa mwenyekiti wao (mzenji) na wazenji watashikilia maoni ya m/mwenyekiti zenji. Nyani na tumbili watakuwa wanajadiliana namba ya kuliendeleza shamba la binadamu, na kwa maajabu binadamu atawaamini!!
 
Back
Top Bottom