Zanzibar: Othman Masoud awataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Unguja kujenga umoja na mshikamano ili Serikali ipambane kuleta maendeleo

Zanzibar: Othman Masoud awataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Unguja kujenga umoja na mshikamano ili Serikali ipambane kuleta maendeleo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Makamu wa kwanza wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud, amewataka wananchi wa mkoa wa kaskazini Unguja kujenga umoja na mshikamano ili kutoa fursa kwa serikali kupambana katika kuleta maendeleo.

Makamu wa kwanza ameyasema hayo mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea baadhi wagonjwa na wananchi wenye matatizo mbali mbali waliomo katika mkoa wa huo wa kaskazini unguja.

Mheshimiwa Othman amesisitiza kwamba kama alivyoirithi nafasi ya Umakamu wa kwanza kutoka kwa mtangulizi wake Marehem Maalim Seif, basi atahakikisha anawatumikia vyema Wazanzibari ili kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua.

"Lengo letu kama serikali ni kupiga hatua zaidi na kutoka hapa tulipo na kusogea mbele, tena tusogee mbele zaidi panapostahiki, na katika kulifikia hili niwajibu wetu kwa pamoja kushirikiana kuhakikisha hili linafanikiwa" alifafanua

"Umoja na mshikamano ukikosekana katika jamii maendeleo pia hayatakuwa na nafasi, hivyo nijukumu letu kama Wazanzibari kuungana na kuwa kitu kimoja kwa maslahi yetu wote" alitanabahisha

Aidha Mheshimiwa Othman alisema hatoyaangusha matumaini ya Wazanzibari juu yake kwakusisitiza kuendeleza juhudi zilizoanzishwa.

"Kwa yale yote yaliwakuwa yameanzishwa na yale ambayo tunayahitajia kuyaimarisha zaidi, mimi Makamu wa kwanza wa Rais nachukua dhamana na nitahakikisha kwa juhudi na maarifa yangu inshaallah nitawatumikia Wazanzibari na tutafikia malengo" alieleza Mheshimiwa Othman.

Wakazi wa maeneo mbali mbali katika mkoa wa Kaskazini Unguja wamekishukuru kitendo hicho cha Makamu wa kwanza wa Rais, kushuka chini na kuwafariji wananchi wake wakisema kwamba wanaiona thamani yao mbele ya viongozi hao wakuu.View attachment 1764268View attachment 1764269View attachment 1764270
IMG-20210426-WA0002.jpg


Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Wazanzibar wanaishi kama yatima. Very sad 😔😔😔 muungano hauna faida kwao.
 
Back
Top Bottom