dada white
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 1,228
- 514
Padri Evarist Mushi, ambaye ni paroko wa parokia ya Minara Miwili - Mtoni Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana leo mida ya saa moja asubuhi akielekea kanisani kuongoza ibada.
Source: Radio Wapo
---
Padre E. Mushi Paroko wa parokia ya Minara Miwili Mtoni Zanzibar ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika asubuhi hii.
Ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ghafla ilitokea gari ndogo na waliokuwamo ndani ya gari ile wakamrushia risasi.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano.
Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.
PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana