Pre GE2025Zanzibar: Polisi wakanusha taarifa ya Mjumbe wa Kamati Kuu ACT kudaiwa kutekwa na vyombo vya ulinzi, wasema alikamatwa na kuachiwa kwa dhamana
Mapema leo Naibu Katibu Mkuu wa ACTWazalendo -Zanzibar Omar Ali Shehe alidai kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Hadija Anuwar alitekwa na watu wasiyojulikana wakati wa uandikishaji katika Daftari la kudumu la Tume ya Uchaguzi Zanzibar -ZEC.
Jeshi la polisi limetoa ufafanuzi wa tukio hilo likisema Khadija alikuwa na dhumuni la kuzorotesha zoezi la uandikishaji daftari la kudumu, ambapo alikamatwa na kuachiwa baadaye kwa dhamana.
Kwani mwenye uwezo wa kufanya haya ni nani?.
Hivi unaweza kuja na ushujaa tena na gari zozote kisha mkanushe.
Kweli ushuzi na haja kubwa zijawai kuwa na ushirikiano ila zina ushirikiano kwenye ushiriki wa utumbo mkubwa.