Zanzibar: Polisi watolea ufafanuzi sakata la Mauzinde kukatwa masikio

Zanzibar: Polisi watolea ufafanuzi sakata la Mauzinde kukatwa masikio

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja limetolea ufafanuzi juu ya tukio la kushambuliwa kwa Kijana Mmoja anayefahamika kwa jina la Maulid Hussein Abdallah maaraufu Mauzinde

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi SACP Daniel Shilla wakati akizungumza na waandishi wa habari

Kamanda Shilla amesema tukio la kutekwa kwa kijana hilo limefanyika Juni 02, mwaka huu huko Kibele ambapo kijana huyo alikatwa sehemu ya chini ya masikio yake huku akisema kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana

Pia soma:
- Watu wasiyojulikana wamshambulia Mauzinde kwa kumkata masikio na kumtelekeza msituni
 
Back
Top Bottom