Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Kama hivi haya ndo maandalizi ya Uchaguzi au nini?
======================================================
Serikali imetoa Sh209 milioni kwa vikundi 18 vya vijana ili kusaidia ujasiriamali na biashara kupitia asilimia 10 ya mapato ya Serikali za mitaa. Vikundi hivyo, vyenye wanachama 134, vinajumuisha wanawake (4%), vijana (4%), na watu wenye ulemavu (2%).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff, amesema Serikali imeanzisha programu maalumu ya mikopo kwa makundi haya ili kupunguza changamoto ya ajira. Alitoa kauli hiyo leo, Februari 24, 2025, akijibu swali la Mwakilishi wa Mwanakwerekwe, Ameir Abdalla Ameir.
"Hadi Desemba mwaka jana, jumla ya vikundi 18 vya vijana vyenye wanachama 134, kati yao wanaume 93 na wanawake 41, vimepatiwa mikopo ya Sh209 milioni kwa lengo la kuimarisha shughuli zao za ujasiriamali na biashara ili kujiajiri," amesema Shariff.
Pia, amesema hivi karibuni wameanzisha programu ya kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu katika masuala ya ujasiriamali. Programu hiyo itawafundisha wanafunzi hao masuala ya ujasiriamali na kubuni mawazo ya kibiashara ili kuanzisha shughuli zao za kiuchumi wanapohitimu chuo.
Waziri Shariff amesema programu hiyo ilizinduliwa Novemba mwaka jana na ilihudhuriwa na wanafunzi 227 wanaosoma fani mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuwawezesha vijana kujiajiri katika shughuli zao za uzalishaji kupitia uchumi wa buluu na mafunzo ya amali.
Akijibu swali la nyongeza, Waziri Shariff amesema wengi wanakosa mikopo hiyo na kujiendeleza kwa sababu wanapoipata wanaitumia kinyume na mawazo waliyoyainisha katika uombaji, na ndiyo sababu wanashindwa kurejesha mikopo ikifika wakati wa urejeshwaji.
Source: Mwananchi