Ningependa tutofautishe kati ya nchi,taifa na dola ili tujadili vizuri Tanganyika.league of nations baada ya wajerumani kuangukia pua WW1 waliwapa dhamana ya kutawala eneo(nchi)lilikuwa koloni la wajerumani likijulikana kama german east africa,likijumuisha Tanzania bara kama tunaivyotambua sasa,na eneo la Ruanda-Urundi ambalo ni nchi za Rwanda and Burundi kama zinavyotambulika sasa.Dhamana hiyo ya utawala,ilpelekea waingereza sasa kuwa na dola(state)mpya ambayo haikuwa sovereign,isiyo na madaraka kamili,ikiwa chini ya dola ya uingereza.
na baada ya ya WW2,mandate ya league of nations ikarithiwa na united nations kupitia kwenye trusteeship council ya umoja wa mataifa.kwa hiyo uingereza iliendelea tena kusimamia ardhi,na dola waliyoitengeneza kwa ajili ya utawala,kwa niaba ya umoja wa mataifa.kwa hiyo nchi ya tanganyika ipo tangu duina iumbwe,imeitwa majina tofauti,imekuwa sehemu ya mataifa tofauti,lakini mipaka yake ya sasa na jina hili,imeanza mwaka 1922.
sasa eneo hili(nchi)ambalo waingereza waliendeleza dola mpya ya tanganyika,baada ya ruanda urundi kupewa mandate wabelgiji,nadhani mgao ulizingatia ukaribu na nguvu ya ushawishi,kenya na uganda walikuwepo uingereza,DRC walikuwepo wabelgiji,ingawa wareno walikuwepo msumbiji,ndhani nguvu yao ilikuwa mgogoro.mpaka tunashughulikia uhuru wa dola ya tanganyika,inayomiliki nchi ya tanganyika ya mipaka ya tanzania bara,tulikuwa na mataifa(jamii za watu wenye asili,utamaduni,utawala,lugha,eneo lenye mipaka,mfumo wa usuluhishi na lengo moja)yanakaribia 100.wakati dola ya tanganyika inaingozwa na waingereza,haikuwa nia yao kuunganisha haya mataifa ili liwe taifa moja la tanganyika,waliyaita makabila,kama walivyoitwa wao na warumi,na wakaendelea kupepea muendelezo wa zile tawala za mataifa ya awali,ili mradi tu zinatii amri ya utawala wao,kwa hiyo waka divide and rule,waka hakikisha viongozi wa yale mataifa wanapata privilege na sifa OBE zilkuwa kadhaa,ili dola hii isije kuwa taifa,likawa na nguvu kubwa mpaka ishindikane kutawala.utaona taifa moja kule kilimanjaro ambalo lilikuwa na nguvu,lilianza jitihada zake kudai uhuru wake peke yake.ambayo ni sawa tu.kuna taifa lingine nadhani kule arusha lilifikiria uwezekano huo.vuguvugu la kupatikana uhuru ndio mwanzo wa kuanza kufikria utaifa wa watanganyika,lakini mwanzo mkazo ulikuwa sana kwenye uhuru,kuliko utambulisho wa watu.tulijiona ni kama watu wasiofahamiana wametekwa na jambazi mmoja,basi tushirikiane tumpige kwanza mwizi.lakini siku zilivyokuwa zinazidi kwenda,na watu wa mataifa haya tofauti walivyokuwa wanakutana,kwenye elimu,michezo,biashara na kazi,na nia ya uhuru kuongezeka,nia ya utaifa nayo ikaja.lakini mtu ambaye kwa maoni yangu amechangia sana kwenye kutengeneza taifa la tanganyika ni mwl Nyerere,muono wake ulikuwa kwamba haya mataifa yooote yawe watu wamoja,tujenga taifa moja,tujitengenezee misingi,mwelekeo,hatima kama watu wamoja,kueleka uhuru,na kitambo baada ya uhuru alielekeza nguvu zake nyingi sana,kwenye ujenzi wa taifa,sio kutufanya kuwa ethnically homogeneous,hapana,traits,mtazamo,dhamira,utambulisho,mwelekeo,utamaduni,lugha,desturi...kwa hivyo yeye mchango wake ndio mie naouona mkubwa kuliko watu wengine kwenye kujenga taifa la tanganyika.tarehe ya uhuru ni 9 desemba 1961,lakini hiyo ni tarehe ya dola ya tanganyika kupewa uhuru,jitihada za kuunda taifa la tanganyika,tunaweza kuziweka sambamba na active political mobilization period,miaka ya kati ya hamsini.kujenga taifa ni kazi kubwa sana,inataka consistency time,undertsnading commitment,ambavyo ni haba siku hizi.baada ya muungano,jitihada za ujenzi wataifa zikawa za kujenga taifa tanzania,tukafundishwa uzalendo na kuchanganywa kama karata,tukapelekwa jeshini huko tujuane vizuri,tuwe wamoja.ila sasa tumechoka kuwa taifa tanzania,tunataka kurudi kwenye taifa tanganyika ambalo halipo,kwani hata taifa tanzania halijatengemaa.bado..zanzibar.?