Zanzibar Update 07/06/2021

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Nitaendelea kusimamia utawala bora nchini kwalengo la kufufua maendeleo ya Zanzibar yatakayowainua wananchi kiuchumi - Othman Masoud


Mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wenzake wa ACT wazalendo ngazi ya mkoa, majimbo na matawi katika mkoa wa kichama wa Micheweni, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni.

Aidha amesema uwepo wa tatizo hili kwa muda mrefu ni chanzo cha kuirudisha nyuma Zanzibar kufikia maendeleo,hivyo amesisitiza kuwa ataendelea kusimamia hilo kwa lengo la kutimiza adhma ya serikali ya kuinua uchumi wa wananchi.

"Kujenga misingi imara ya ufuatwaji wa sheria za nchi,ndio msaada mkubwa kwa Zanzibar kufikia malengo hasa katika uwekezaji utakaopunguza tatizo la ajira kwa vijana nchini" alielezea.

Sambamba na hayo amewahimiza wanachama hao kuendelea kuwa na subira katika kipindi hichi cha ujenzi wa nchi,ili serikali iweze kufikia malengo yake.

Katika kikao hicho Mheshimiwa Othman, amepokea wanachama wapya wa ACT Wazalendo, pamoja na kushuhudia zoezi la ulipaji wa kadi za uanachama.

Makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ndugu Juma Duni Haji, amewasisitiza wanachama na viongozi hao kusimamia haki zao ikiwemo vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa, na kutoa taarifa kwa viongozi dhidi ya wahusika wanaokwenda kinyume na agizo la serikali kwa kuzuia kutolewa kwa vitambulisho hivyo.

Nae katibu wa Oganaizesheni na wanachama wa ACT Wazalendo, ndugu Omar Ali Shehe,amewasisitiza viongozi wa mkoa huo kuendelea kuimarisha chama chao ikiwemo kukusanya taarifa za wanachama hai pamoja na kuhamasisha kuingiza wanachama wapya ili kufikia malengo ya chama hicho.

Wakati huo huo mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Mheshimiwa Othman ameendelea na ziara yake hio katika mkoa wa Wete kichama kwa kukutana na viongozi na wanachama wa chama hicho kwa lengo la kutambulishana pamoja na kuzungumza nao.

Akiwa Wete, Mheshimiwa Othman, amewaeleza wananchi kuwa na suala la masheikh kutoka Zanzibar ambao wapo rumande,serikali inaendelea na taratibu,na kupelekwa mahakamani kwaajili ya kusikilizwa kwa kesi yao ni miongoni mwa juhudi zilizofanywa na serikali.

Sambamba na kuwatoa hofu wananchi juu ya bei ya karafuu kwa kuwaambia, "serikali haijashusha bei ya karafuu, bali changamoto huanzia katika soko la dunia".Nakumalizia kwakusema Serikali inapambana kurudisha heshima ya zao hilo na ya nchi kwa ujumla.View attachment 1811807View attachment 1811808View attachment 1811809View attachment 1811810

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Mwende tu tutengeneza katiba ya kuuvunja huu muungano, watu wa bara we are sick of it.

Hivi Zanzibar mnachangia nini bara, we can get the same things without you. Vunja tuu huu muungano hatuutaki hata sisi wabara.

Muungano gani we are giving more than we are getting, uvunjwe.

Huo ni muungano wa CCM tu it’s about time uvunjwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…