Kila mtu aheshimiwe! Si wazanzibari tu bali kila mtu.
Muungano una matatizo na ni vizuri yakatatuliwa kuliko kuyaacha matatizo yatakuwa makubwa zaidi.
Mimi ni mtanganyika. Nitapigania kwenye haki na nitaipigania Tanganyika.
Leo nitajiongelea kiubinafsi kwa kauli ya umimi. Mimi sina chama wala si mtu wa vyama. Mimi nipo pamoja na Lissu.
Lissu kwenye mambo ya muungano alianza kuizungumzia Zanjibar na kwa sasa anazungumzia kadhia za Tanganyika.
Hapa mchawi ni mmoja tu! Ni CCM. CCM ndiyo ambayo inapandikiza chuki. CCM ndiyo ambayo itakayovunja umoja wetu. Kwa sababu inayo nguvu na mamlaka ya kurekebisha haya ambayo kimsingi ndiyo chanzo cha wewe kuleta huu uzi.
Hivyo hapa wa kumshurutwisha ni CCM. Hii hali ikibaki hivi si nzuri.