Zanzibar: Wamiliki wa Hotel kuchukuliwa hatua ikiwa wageni wao watatoka bila kuvaa stara

Zanzibar: Wamiliki wa Hotel kuchukuliwa hatua ikiwa wageni wao watatoka bila kuvaa stara

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1614641789549.png

Serikali ya Zanzibar imesema itawachukulia hatua wamiliki wa hoteli ambao wageni wao watatoka hotelini wakiwa hawajavaa nguo za stara. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale amewataka wageni hasa watalii kutovaa nguo zinazokiuka maadili wawapo maeneo ya umma, mfano sokoni.

Chanzo: Swahili Times
 
Rafiki zangu walifanya kazi Arabuni nako walitakiwa kufanya hivyo. Kwenye compound mnayoishi unatembea unavyotaka lakini kwenda mjini na madukani ni lazima ufunike kichwa mwanamke na nguo istiri maungo. Wanaume pia huwezi kutembea tumbo wazi.
 
Zanzibar wana utamaduni wa kiislamu, nadhan hili ni jambo la kutegemewa + kueleweka na si la kushtukiza

Mwaka 2010, nlitua pale Imam Ally khomein International airport nikashuhudia mdada mzungu wamekataa kumruhusu kisa hana mtandio.
 
Sawa, isiwe tabu: sie watalii tunakuachia nchi yako, tutatembelea comoros, mwambasa, lamu na mozambique
 
Zanzibar wana utamaduni wa kiislamu, nadhan hili ni jambo la kutegemewa + kueleweka na si la kushtukiza

Mwaka 2010, nlitua pale Imam Ally khomein International airport nikashuhudia mdada mzungu wamekataa kumruhusu kisa hana mtandio.
Sawa
 
Tushukuru kuwa watalii wanapenda utofauti hivyo kuvaa ushungi kunaweza kuwa utofauti kwao na wakavaa si kwasababu wanaogopa sheria bali ni sehemu ya utalii.
 
Aaagh visheria uchwara kwenye ulimwengu wa utandawazi ni kichekesho,wazanzibar wana unafiki sana,wanajitia watu wa kushika dini ila kiuhalisia hawapo hivyo

Wadau wa Bububu,mchambawima na mkokotoni nadanganya?
 
Waziri wa maliasili na utalii amesema kwamba Zanzibar itawapiga faini watalii wasio vaa vizuri kwenye maeneo ya beach na mahotelini.

Watalii wale wanao vao vichupi wakiwa maeneo ya beach wanatakiwa kuwaheshimu wanyeji wao . Pia adhabu ya dola 700 itatolewa kwa TOUR guide ambaye hatawashauri wateja wake katika uvaaji.

Nasema hivi pigeni faini hao wataliii lakini mjiandae kuwatafutie ajira hao tour guide na wenye mahoteli
 
Safi sana. Utalii ni habari nyingine na mavazi ni habari nyingine, watalii wanapaswa kuheshimu mila, tamaduni na desturi za maeneo wanayotalii. Ndio maana nchi za wenzetu wanalinda sana taratibu, desturi na mila zao na bado utalii uko pale pale.
 
Back
Top Bottom