Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walishatengeneza Katiba inayokiuka Katiba ya JMT, Nchi yao ndogo(ni wachache sana) hatuwezi kugawana madaraka sawa
Sovereignity is not determined by neither demography nor territory
Walishatengeneza Katiba inayokiuka Katiba ya JMT, Nchi yao ndogo(ni wachache sana) hatuwezi kugawana madaraka sawa
Kuna mambo ni kujitakia!
Kwanini watanganyika wasiandamane kuukataa muungano??????
Huo mkataba wa muungano ni dhulma iliyopitiliza kiasi kwamba hata binamu zetu walioko tanganyika nao hawautaki pamoja na muswada huu wa rasimu ya katiba mpya wa ghiliba unaotaka kupenyezwa tena!Katika makala yake yaitwayo "Nyerere Alitunusuru" yaliyochapishwa katika Gazeti la Sura ya Mtanzania la kuanzia 10/10/13 Comred Ali Sultan ameandika:
Karume hakuwapenda ‘Wasomi', na hakuwa akiwaamini kabisa. Hata ukiangalia wengi wa Viongozi wa ASP waliofungwa na Karume walikuwa ni wale Wasomi, kama Othman Shariff.
Hapana shaka kuwa Comred Ali Sultan alimjua vizuri Karume kwani alikuwa naye katika "Baraza la Mapinduzi" na aliwahi hata kuwa Waziri wa Ilimu wakati wa utawala wa Karume.
La muhimu hapa ni kuwa Raisi Karume alikuwa hakusoma, hakuwapenda wasomi na hakutaka ushauri wa wasomi hata juu ya mambo ambayo yaliwahitajia wasomi kuyasoma kuyachambua, kubadilisha na hata Kumshauri Rais ayakatae iwapo wanayaona yataleta athari mbaya kwa Zanzibar.
Si Ali Sultani tu bali muhimu kwa Wazanzibari ni kuwa Nyerere pia aliujua upungufu huu wa Karume na kuutumilia upungufu huo kumtilisha saini mambo ambayo Karume, kwa hakika hakuyajua athari zake baadaye. Nyerere kwa ilimu yake na kwa ujanja wake, kwanza alifanya mazingaombwe ili Karume amwondoshe Dorado, ambaye alikuwa Mwanasharia mkuu wa Serikali ya Zanzibar, asihudhurie mikutano muhimu na hivyo kumnyima Karume usia mwema na wa lazima katika mikataba yote muhimu, na huu wa muungano ndio uliokuwa muhimu kabisa wakati huo.
Nyerere alimtumilia Karume saikolojia kumtilisha sahihi mambo aliyokuwa hakuwa na kipawa cha kuelewa athari zake siku za siku za mbele. Haya mawili pekee yanatosha kuufanya mswada wote wa muungano "nul and void" yaani batil, au kuwa hauna uhalali wowote mbele mahkama yenye kufuata sharia za haki na uadilifu.
Hapana shaka yoyote, ukipeleka kwenye mahakama yenye kuamua kwa haki na uadilifu, ni mara moja itaamua kuwa yote aliyoyasaini Karume kuwa ni batil. Kila mwana sharia anayeelewa maana ya haki na uadilifu anayaelewa haya.
Ukiongeza pia kuwa Karume hakupata idhini ya Wazanzibari kwa kura ya maoni kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika ndiyo kabisa aliyoyatia saini yake hayakuwa na uhalali.
Nchi huunganishwa kwa njia mbili, moja ni ya kuulizwa wananchi kama wanautaka muungano ama la. Wasipoutaka, muungano hauwezi kuwa.
Wazanzibari hawakushauriwa na hili pia linaufanya mkataba wa muungano na muungano wenyewe "nul and void" kisharia.
Njia ya pili ni ya kuiteka nchi kijeshi, na njia hii pia haikubaliki kisharia.
Njia ya tatu ni ya Kinyerere na wafuasi wake, ya kuiteka nchi kwa ghilba, kidogokidogo kama panya anavyokula nyama ya aliyelala kwa kutafuna na kupuliza. Hili pia halikubaliki.
Kwa Wazanzibari kuzungumzia kipengee cha mkataba batil kama kwamba mkataba wenyewe una uhalali ni kujitia katika mitego ya Nyerere na wafuasi wake.
Iwapo tunakubaliana kuwa Karume hakufahamu alichokisaini, hakujua athari zake, na mawakili wake waliokuwa na uwezo wa kuelewa na kumshauri ipasavyo walifanyiwa mazingaomwe na Nyerere hata wakatolewa kwenye mikutano ili ipatikane saini ya Karume kwa wepesi inaufanya mkataba huo kuwa batil.
Na mkipeleleza mtaona pia baada ya hapo pia sehemu nyingi za kuinyima Zanzibar haki zake ziliongezwa kinyemela.
Wafuasi wa Nyerere wanategemea kuwa madamu kuna mswada na ndani yake kuna sharia hizo, basi sharia hizo ni za kihalali hata iwapo zimepatikana kwa udanganyifu na ghilba.
Ni juu ya Wazanzibari na waliondugu zao wa kweli walioko Tanganyika kuhoji na kuukataa mkataba ulipatikana kwa ghilba na bila ya kushauriwa wananchi wahusika.
Jaribu ufikirie kuna nduguyo ambaye hakusoma na ana shamba lake anakodisha na anategemea kupata pato la kumwendeshea maisha yake kutokana na mali yake hiyo; akaja mtu akamvuta pembeni na kumwambia mimi nitakupa shilingi kadha wa kadha unikodishe shamba lako lakini sharti yangu uutie saini yako mkataba huu, bila ya kumshauri nduguyo aliyesoma kwani nduguyo mkorofi sana na hakutakii kheri, ni mimi ninayekutakia kheri na utafaidika pakubwa ukitia dole lako kama ni saini ya kuukubali mkataba huu.
Jee, wewe nduguye ukaja ukamwona nduguyo anafukarika kwa kunyang'anywa kwa ghilba mali yake na mjanja kwa sababu kamtilisha saini yake huku hajui kuwa mkataba ulikuwa na vipengee vya kumyang'anya nduguyo haki zake, utaukubali mkataba kama huo uliojaa dhulma uliosainiwa na nduguyo aliyekuwa hakusoma na hakufahamu sawasawa nini anachokisaini?
Jee, mktaba huo utakubaliwa katika mahkama yenye kufuatilia haki na uadilifu? Lakini hivyo ndivyo wanavyoshikilia maloya wa Nyerere katika kutaka kudhulumu haki na mali za Zanzibar
. Si mnawaona wanakakania kuwa maliasilia ni haki ya Tanzania na si ya Zanzibar ingawa mali hayo yako Zanzibar!
Sovereignity is not determined by neither demography nor territory