JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Kamishna wa Polisi, Awadhi Juma Haji amewaonya wapelelezi wanaokwamisha kesi za dawa za kulevya Zanzibar kuwa jeshi hilo halitakuwa na muhali kwa maafisa hao na kusisitiza ueledi katika majukumu yao.
Kila mpelelezi awajibike kufuatilia jalada lake hatua kwa hatua, ni marufuku kukumbatia jalada la polisi, mwendesha mashitaka akimaliza kazi yake ahakikishe jalada hilo limerejeshwa polisi mara moja ili nao waendelee na hatua nyingine.
“Kuna mashauri yanaondolewa Mahakamani kwa kuwa yamechukua muda mrefu kukamilisha upelelezi, tunabaini jalada hilo halijarudishwa Polisi kwa muda mrefu na baadhi ya waendesha mashitaka wamekuwa wakikaa nayo,” – Haji.
Chanzo: ITV