Zanzibar wapendekeza Mambo matano yatolewe katika Muungano

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,013
Micheweni. Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wametoa mapendekezo ya pamoja wakitaka mambo matano yaondolewe kwenye Muungano, yabaki kwenye Serikali washirika.

Waliyopendekeza yaondolewe ni Mambo ya Nje, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki kuu, usajili wa vyama vya siasa pamoja na ushuru wa bidhaa wakisema kwamba kama yataendelea kuwepo kwenye Muungano kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatasababisha Serikali shirikishi kuwa dhaifu.Wakizungumza baada ya kuwasilishwa kwa kazi za makundi yaliyopewa jukumu la kujadili suala la mihimili, wajumbe hao walisema mambo hayo matano ndiyo yanayoweza kuzipa nguvu Serikali shirikishi ambazo zitakuwa Tanganyika na Zanzibar.

Walitolea mfano wa mambo ya nje na kusema kuwa ikiwa Rais wa Serikali ya Tanganyika au Zanzibar ataondolewa jukumu la kuteua mabalozi na hata kuiwakilisha nchi nje ya nchi atakuwa ameondolewa meno. “Nchi washirika ziachiwe masuala ya mambo ya nje,”alisema Kassim Mohamed Kassi, mkazi wa Chimba akiwakilisha vijana.

Kuhusu Sarafu na Benki Kuu, walisema sababu za kupendekeza iondolewe katika muungano ni kuwa itadhoofisha uchumi wa nchi washirika.

Aidha kwa upande wa uraia na uhamiaji, walisisitiza kuwa kila nchi watu wake wana utamaduni usioingiliana na nchi nyingine washirika, hivyo kila upande uwe huru.

Ushuru wa bidhaa, wajumbe hao walipendekeza ubaki kwenye nchi washirika na siyo Muungano kama inavyopendekezwa kwa sababu ikiwa itaachwa hivyo sehemu kubwa ya kodi na ushuru kutoka nchi washirika zitashindwa kuwanufaisha watu wake.

Kuhusu usajili wa vyama vya kisiasa, wajumbe hao walisema hiyo ni moja ya kero za muungano iliyojitokeza baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi. Sheria ya chama ili kisajiliwe sharti kipate wanachama wa mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Walitaka mambo ya muungano yabaki mawili tu ambayo ni Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano.
 
Kinachonifurahisha ni kuona kwamba Zanzibar itasaidia sana katika upatikanaji wa Serikali pendwa ya Tanganyika.Huku Bara CCM imeshateka Mchakato Mzima wa Katiba na hivyo kuondoa maana nzima ya upatikanaji wa katiba kutokana na Mawazo huru.
 
Duh! naona jamaa kaweka na sample ya passport kwenye avatar! Mawazo mazuri hayo tusubiri mchakato wa katiba utaamua nini..
 
GHIBUU,

..nadhani kila upande uwe kivyake.

..kwenye suala la ulinzi tunaweza kuwa na mkataba wa ulinzi.

..suala la Katiba haliwezekani kuwa la muungano ikiwa kuna uraia wa Tanganyika na uraia wa Zanzibar.

..You r sending a wrong msg kwa wahusika huku Tanganyika.

..ndiyo maana kuna wakubwa huku wanapendekeza serikali 3 wakifikiri that is what u want. wengine wanafikiri wakiwapendelea ktk muungano kwa nafasi za kazi, madaraka, ubunge, na mgao mkubwa wa bajeti, basi mtatulia ktk mfumo huu wa serikali 2.

cc: gombesugu, takashi, Mchambuzi, Jasusi
 
Last edited by a moderator:

PASPORT.jpg
 
Nakuaminia mkuu, big up....

Ingekuwa amli yangu ningesema muungano kwisha tubaki na udugu wetu wa kawaida lakini kila nchi iwe kivyake. Mimi nawashanga wanao sema kuvunja muunggano ni laana huo ni mtazamo mbaya sana watu wanafunga ndoa kwa gharama kubwa lakini mwisho wasambalatika ndio uwe muungano? jamani kama kuna kazi zingine wacha tufanye lakini hili suala la muungano tunge amua kwa pamoja kuwa umekwisha kwani kila chenye mwanzo kina mwisho.
 
Duh! naona jamaa kaweka na sample ya passport kwenye avatar! Mawazo mazuri hayo tusubiri mchakato wa katiba utaamua nini..

Mkuu Mathcom, nina mashaka tunajisumbua tu na hizi ngonjera za serekali mbili, serekali moja, serekali tatu. Wenzio tayari weshaamua Zanzibar na Tanganyika wote wawili wananyang'anywa mamlaka. Mamlaka Kamili yanabaki kwenye ile Serikali ya Tatu katika Federal State, na passport inafanana na hii ID hapa chini. Hatoki mtu hapa!

FEDERAL ID.jpg

Micheweni. Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wametoa mapendekezo ya pamoja wakitaka mambo matano yaondolewe kwenye Muungano, yabaki kwenye Serikali washirika.

Waliyopendekeza yaondolewe ni Mambo ya Nje, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki kuu, usajili wa vyama vya siasa pamoja na ushuru wa bidhaa wakisema kwamba kama yataendelea kuwepo kwenye Muungano kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatasababisha Serikali shirikishi kuwa dhaifu.Wakizungumza baada ya kuwasilishwa kwa kazi za makundi yaliyopewa jukumu la kujadili suala la mihimili, wajumbe hao walisema mambo hayo matano ndiyo yanayoweza kuzipa nguvu Serikali shirikishi ambazo zitakuwa Tanganyika na Zanzibar.

Walitolea mfano wa mambo ya nje na kusema kuwa ikiwa Rais wa Serikali ya Tanganyika au Zanzibar ataondolewa jukumu la kuteua mabalozi na hata kuiwakilisha nchi nje ya nchi atakuwa ameondolewa meno. "Nchi washirika ziachiwe masuala ya mambo ya nje,"alisema Kassim Mohamed Kassi, mkazi wa Chimba akiwakilisha vijana.

Kuhusu Sarafu na Benki Kuu, walisema sababu za kupendekeza iondolewe katika muungano ni kuwa itadhoofisha uchumi wa nchi washirika.

Aidha kwa upande wa uraia na uhamiaji, walisisitiza kuwa kila nchi watu wake wana utamaduni usioingiliana na nchi nyingine washirika, hivyo kila upande uwe huru.

Ushuru wa bidhaa, wajumbe hao walipendekeza ubaki kwenye nchi washirika na siyo Muungano kama inavyopendekezwa kwa sababu ikiwa itaachwa hivyo sehemu kubwa ya kodi na ushuru kutoka nchi washirika zitashindwa kuwanufaisha watu wake.

Kuhusu usajili wa vyama vya kisiasa, wajumbe hao walisema hiyo ni moja ya kero za muungano iliyojitokeza baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi. Sheria ya chama ili kisajiliwe sharti kipate wanachama wa mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Walitaka mambo ya muungano yabaki mawili tu ambayo ni Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano.
 
Kinachonifurahisha ni kuona kwamba Zanzibar itasaidia sana katika upatikanaji wa Serikali pendwa ya Tanganyika.Huku Bara CCM imeshateka Mchakato Mzima wa Katiba na hivyo kuondoa maana nzima ya upatikanaji wa katiba kutokana na Mawazo huru.

Kuna jamaa yangu kaniambia kuwa kuna kamati ya kuratibu nini kisemwe na wananchi wanapewa script ya kusoma kwenye vikao hivi. Ukweli hata kama wengi wanapenda muungano kwa kuwa wakishawishiwa wanakubali basi tuamue nasi bara kuwa sasa basi TUBAKIE TU NA UJIRANI MWEMA hakuna haja ya hii kitu.

Dhambi ya kumnyima Seif urais na kumpa Mwinyi wakati zengwe alilitengeneza mwenyewe yazidi kuwatafuna CCM. Seif hatokubali hata kidogo
 
Micheweni. Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wametoa mapendekezo ya pamoja wakitaka mambo matano yaondolewe kwenye Muungano, yabaki kwenye Serikali washirika.

Waliyopendekeza yaondolewe ni Mambo ya Nje, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki kuu, usajili wa vyama vya siasa pamoja na ushuru wa bidhaa wakisema kwamba kama yataendelea kuwepo kwenye Muungano kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatasababisha Serikali shirikishi kuwa dhaifu.Wakizungumza baada ya kuwasilishwa kwa kazi za makundi yaliyopewa jukumu la kujadili suala la mihimili, wajumbe hao walisema mambo hayo matano ndiyo yanayoweza kuzipa nguvu Serikali shirikishi ambazo zitakuwa Tanganyika na Zanzibar.

Walitolea mfano wa mambo ya nje na kusema kuwa ikiwa Rais wa Serikali ya Tanganyika au Zanzibar ataondolewa jukumu la kuteua mabalozi na hata kuiwakilisha nchi nje ya nchi atakuwa ameondolewa meno. "Nchi washirika ziachiwe masuala ya mambo ya nje,"alisema Kassim Mohamed Kassi, mkazi wa Chimba akiwakilisha vijana.

Kuhusu Sarafu na Benki Kuu, walisema sababu za kupendekeza iondolewe katika muungano ni kuwa itadhoofisha uchumi wa nchi washirika.

Aidha kwa upande wa uraia na uhamiaji, walisisitiza kuwa kila nchi watu wake wana utamaduni usioingiliana na nchi nyingine washirika, hivyo kila upande uwe huru.

Ushuru wa bidhaa, wajumbe hao walipendekeza ubaki kwenye nchi washirika na siyo Muungano kama inavyopendekezwa kwa sababu ikiwa itaachwa hivyo sehemu kubwa ya kodi na ushuru kutoka nchi washirika zitashindwa kuwanufaisha watu wake.

Kuhusu usajili wa vyama vya kisiasa, wajumbe hao walisema hiyo ni moja ya kero za muungano iliyojitokeza baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi. Sheria ya chama ili kisajiliwe sharti kipate wanachama wa mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Walitaka mambo ya muungano yabaki mawili tu ambayo ni Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano.
sserikali tatu ndio mpango mzima hapo 2
 
Ninachotaka Mkataba, serikali tatu imekuja kutokana rasimu haikutoa fursa ya muvunja muungano,lakini hata hivyo JK alisisitiza kwamba watu wote watoe maoni kama muungano kuuboresha sio kuvunja, tukaja na maoni ya mkataba, na tulikuja na hoja kwa tume ya warioba, na alikiri hilo wakati wa uzinduzi, alisema kwamba zanzibar maoni ya mkataba yalikuwa ni mengi zaidi na hoja za kuaminika, lakini tume yake imependekeza serikali tatu, sasa jee uko uhuru wa maoni na democrasia?

Sisi kama wananchi tunaendelea kutoa maoni yetu, kama tunavyopendekeza maoni hayo, bado tunadai zanzibar yenye mamlaka kamili, tena hapo mutajua wenyewe nyinyi kama mutakuwa na serikali ya muungano au mutataka mkataba, au mutataka serikali tatu, sisi tunachotaka kwa upande wetu zanzibar yenye mamlaka kamili nje na ndani,naunga mkono hoja hizo hapo juu 100 percent, hata hivyo hilo la ulinzi ningeomba nitoe ufafanuzi zaidi, hata kama tutashirikiana suala hilo, zanzibar iwe inalindwa na wazanzibari wenyewe,police, na JESHI LA KULINDA WANANCHI vile vile na usalama.

Kwa UN ,tanzania jeshi la UN lipo lakini ni watanzania wenyewe, nasi kama tutakuwa na ulizi ni suala la muuungano, basi tuwe wazanzibari wenyewe.
GHIBUU,

..nadhani kila upande uwe kivyake.

..kwenye suala la ulinzi tunaweza kuwa na mkataba wa ulinzi.

..suala la Katiba haliwezekani kuwa la muungano ikiwa kuna uraia wa Tanganyika na uraia wa Zanzibar.

..You r sending a wrong msg kwa wahusika huku Tanganyika.

..ndiyo maana kuna wakubwa huku wanapendekeza serikali 3 wakifikiri that is what u want. wengine wanafikiri wakiwapendelea ktk muungano kwa nafasi za kazi, madaraka, ubunge, na mgao mkubwa wa bajeti, basi mtatulia ktk mfumo huu wa serikali 2.

cc: gombesugu, takashi, Mchambuzi, Jasusi
 
GHIBUU,

..semeni mnataka kuwa HURU.

..masuala ya mkataba yafuatie baada ya Zanzibar kuwa huru.

..siyo lazima kuwa na mkataba na Tanganyika.

..Kenya ni majirani na ndugu wa Znz, kwanini hampendekezi kuwa na mkataba nao?

..wakati mwingine mnatutisha na hii hoja yenu ya mkataba ambao hauko wazi.

cc Nguruvi3, takashi, Foum Jnr, gombesugu

Wewe hutaki tanganyika huru na kujiunga na rwanda?
 
GHIBUU,

..semeni mnataka kuwa HURU.

..masuala ya mkataba yafuatie baada ya Zanzibar kuwa huru.

..siyo lazima kuwa na mkataba na Tanganyika.

..Kenya ni majirani na ndugu wa Znz, kwanini hampendekezi kuwa na mkataba nao?

..wakati mwingine mnatutisha na hii hoja yenu ya mkataba ambao hauko wazi.

cc Nguruvi3, takashi, Foum Jnr, gombesugu
JokaKuu, wanasema ulinzi na usalama liwe suala la muungano! Sasa huyo rais atakayekuwa na jeshi atakuwa Amir jeshi wa nchi gani?
Maana kwa jinsi wanavyopendekeza wao kila mshirika*(hakutakuwa na mshirika kwa jambo moja) awe na wizara yake ya mambo ya nje, kiti chake UN n.k. sasa amir jeshi atakuwa na kazi gani au majukumu gani.

Ukisoma mawazo hayo ni wazi Maalim Seif kawatuma. Hilo halina tatizo kwasababu hata Nape Nnauye naye kawatuma wake. Suala la kujiuliza hivi rais wa znz kwanini atake ulinzi wa Tanganyika? Nasema ulinzi wa Tanganyika kwasababu jeshi ni la Tanganyika! period!

Hakuna mamlaka kamili kama unalala na kulindwa na jeshi la nchi nyingine.
Wao wanatakiwa wawe na jeshi lao kwanza halafu mamlaka kamili, lakini wakitaka tuwalinde basi tutawalinda kama tufanyavyo kagera na singida.

Pili, huo ulinzi na usalama wao watachangia nini? au wanataka 'umeme' mwingine?

Hapa nadhani ni kuvunja muungano maana huo upuuzi wa mkataba ni wa Seif na wznz.
Kitu kinachosikitisha ukimuuliza Ghibuu Mkataba ni kitu gani hawezi kukueleza.
Tanganyika tunasema mkataba uanadikwe lakini mwisho ni chumbe, ukivuka chumbe basi uambatane na kitambulisho alichochukua maalim seif Karimjee. Hajarudisha anacho, halafu anataka mamlaka kamili.

Wznz acheni kuhangaika, njia ni moja tu, mdai kura ya maoni halafu mpige kukataa muungano. Hapo mtakuwa mumemaliza kila kitu.

Eti katiba iwe jambo la muungano! katiba inakuwaje jambo la muungano kama ina jambo moja tu la ulinzi na usalama.
Hivi kuna sababu ya kuandika katiba yenye jambo moja.

Wao waamue maana sisi tushaamua Tanganyika itarudi.
 
Last edited by a moderator:
Micheweni. Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, wametoa mapendekezo ya pamoja wakitaka mambo matano yaondolewe kwenye Muungano, yabaki kwenye Serikali washirika.

Waliyopendekeza yaondolewe ni Mambo ya Nje, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki kuu, usajili wa vyama vya siasa pamoja na ushuru wa bidhaa wakisema kwamba kama yataendelea kuwepo kwenye Muungano kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatasababisha Serikali shirikishi kuwa dhaifu.Wakizungumza baada ya kuwasilishwa kwa kazi za makundi yaliyopewa jukumu la kujadili suala la mihimili, wajumbe hao walisema mambo hayo matano ndiyo yanayoweza kuzipa nguvu Serikali shirikishi ambazo zitakuwa Tanganyika na Zanzibar.

Walitolea mfano wa mambo ya nje na kusema kuwa ikiwa Rais wa Serikali ya Tanganyika au Zanzibar ataondolewa jukumu la kuteua mabalozi na hata kuiwakilisha nchi nje ya nchi atakuwa ameondolewa meno. “Nchi washirika ziachiwe masuala ya mambo ya nje,”alisema Kassim Mohamed Kassi, mkazi wa Chimba akiwakilisha vijana.

Kuhusu Sarafu na Benki Kuu, walisema sababu za kupendekeza iondolewe katika muungano ni kuwa itadhoofisha uchumi wa nchi washirika.

Aidha kwa upande wa uraia na uhamiaji, walisisitiza kuwa kila nchi watu wake wana utamaduni usioingiliana na nchi nyingine washirika, hivyo kila upande uwe huru.

Ushuru wa bidhaa, wajumbe hao walipendekeza ubaki kwenye nchi washirika na siyo Muungano kama inavyopendekezwa kwa sababu ikiwa itaachwa hivyo sehemu kubwa ya kodi na ushuru kutoka nchi washirika zitashindwa kuwanufaisha watu wake.

Kuhusu usajili wa vyama vya kisiasa, wajumbe hao walisema hiyo ni moja ya kero za muungano iliyojitokeza baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi. Sheria ya chama ili kisajiliwe sharti kipate wanachama wa mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Walitaka mambo ya muungano yabaki mawili tu ambayo ni Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano.
Hizi hoja za kutoka Zanzibar nazo zina mashaka kwelikweli, hata utajiuliza anayetoa anaelewa anachosema au ndio anasema tu. Kwenye red:- Wakati wataalamu wa uchumi wanakubaliana kuwa Umoja wa Fedha chini ya Sera ya Pamoja ya Fedha (Monetary Policy) kwa nchi zenye mahusiano ya biashara hupelekea ufanisi katika biashara na hivyo uchumi, hawa wanasema hili litadhoofisha uchumi (msingi wa kuboresha biashara na uchumi ni kwamba inachangia katika price stability, wider financing options, reduce exchange rate fluctuations, easy factor mobility and support economic growth & employment). Sijui uchumi wa wapi huu wa hawa wazanzibar, majanga haya. Lakini cha ajabu ni kwamba Tanzania kama nchi inajadiliana na nchi nyingine kuwa na Sera moja ya Fedha, wao wanataka hiyo nchi moja iwe na sera mbili tofauti za fedha, Barazil na China zinafikiria kuwa na fedha moja ili kukuza biashara, na uchumi, wao wanasema fedha ya pamoja inadhoofisha uchumi; sijui hawaelewi hata kinachoendelea duniani?

Kwenye Blue, msingi mkubwa wa Muungano ni uraiya vinginevyo unakuwa si muunggano bali ushirikiano wa kibiashara, (vilevile hata kama ni ushirikiano wa kibiashara, kupunguza masharti ya uraiya na kuufanya kama ni mmoja ndio hitajio kuu la kufikia lengo la ushirikiano) sasa wao wanasema hili hapana; sasa hata huelewi wanataka nini? Maana sisi watanganyika tuko wazi kabisa, ima daini kura ya maoni ya kujitoa katika Muungano completely au bakini tutakavyo, sio blabla za sokoni. Hata hivyo, kwa hoja hii, muanze maandalizi ya kuwapokea watu wenu, msije kusema mmeshtukizwa muda mfupi ujao.

Hiyo ya mwisho, ni umbumbumbu wa kutoelewa tu mambo ya ushuru wa bidhaa, maana hata haieleweki. Zanzibar by nature ni import-based country, haina production ya kutosha na ina population ndogo, hivyo iwapo itakuwa na ushuru wake na lets say kuweka kuwa juu sana, itaumiza tu watu wake na Tanganyika haitaumia kwa sababu ni nchi kubwa by production and consumption (Small& large country tariff analysis case). Na wakiweka kuwa wa chini sana, bidhaa hazita-flood kwa sababu hakuna population kubwa ya ku-absorb all imported commodities na itakuwa iko na taratibu tofuati za ushuru na Tanganyika hivyo hakutakuwa na chance ya kuuzia Tanganyika bidhaa zilizokuwa imported kupitia Zanzibar(Kutakuwa na kulipia kodi mara mbili) na hivyo automatically, wafanyabiashara hawatakuwa na sababu ya kushushia mizigo yao Zanzibar na kisha kusafirisha Tanganyika; kwani ni hasara, gharama na kupoteza muda. Jipangeni mdai kura ya maoni kuvunja Muungano ndiyo suluhu ya kudumu ma-Akhiy zangu.
 
Ndugu yangu hivi ulikuwa unafuatilia mchakato mzima wa katiba mpya zanzibar toka ulipoanza ? Mbona taratibu zote tumeshachukua sisi kama wananchi, suala hilo Shein hatoweza kufanya hata siku moja kutokana analinda madaraka yake alio pewa na watanganyika kiutawala zanzibar na kuwa kibaraka chenu, ndio ukaona Uwamsho mpaka leo wako rumande wanateseka hata makosa yao hayana kichwa wala mguu, Uwamsho wamefanya kazi kubwa kuwaamsha wazanzibar kudai zanzibar HURU.

Kama kweli watanganyika muko tayari kuiwacha zanzibar, mshindikizeni Warioba babu yenu abadilishe mswada wa sheria itoe fursa kutoa maoni ya kuvunja muungano,au kutoa fursa ya kura ya maoni kujitenga.

Sisi hatuhofii chochote katika suala la kujitenga, wala usidhani kwamba eti dar es salaam na mikoa mingine kuna wapemba ndio tuna hofu, hilo suala haliiiingiliani kabisa katiba suala la nchi, kila mwananchi ana haki ya kuishi popote duniani alimuradi anafuata taratibu za hichi hizo.

Na pia ile hoja yenu kwamba munatupa umeme bure hilo halina mashiko, tutaendelea na miakta ya kuuziana umeme, kama mutanuna kisa tunavunja muungano na kutukomoa, hilo halina tatizo tunayo magenerator ya kutosha zanzibar mapya kabisa kwa ajili ya maafa yoyote kutusukumia siku.

Sisi badai yetu zanzibar huru, nje na ndani, kama mkataba ije baada ya kuwa huru, lakini kutokana na mfumowa sheria tumeishia kwenye tatu.

Tunachotaka tupumueeeee
GHIBUU,

..semeni mnataka kuwa HURU.

..masuala ya mkataba yafuatie baada ya Zanzibar kuwa huru.

..siyo lazima kuwa na mkataba na Tanganyika.

..Kenya ni majirani na ndugu wa Znz, kwanini hampendekezi kuwa na mkataba nao?

..wakati mwingine mnatutisha na hii hoja yenu ya mkataba ambao hauko wazi.

cc Nguruvi3, takashi, Foum Jnr, gombesugu
 
Hizi hoja za kutoka Zanzibar nazo zina mashaka kwelikweli, hata utajiuliza anayetoa anaelewa anachosema au ndio anasema tu. Kwenye red:- Wakati wataalamu wa uchumi wanakubaliana kuwa Umoja wa Fedha chini ya Sera ya Pamoja ya Fedha (Monetary Policy) kwa nchi zenye mahusiano ya biashara hupelekea ufanisi katika biashara na hivyo uchumi, hawa wanasema hili litadhoofisha uchumi (msingi wa kuboresha biashara na uchumi ni kwamba inachangia katika price stability, wider financing options, reduce exchange rate fluctuations, easy factor mobility and support economic growth & employment). Sijui uchumi wa wapi huu wa hawa wazanzibar, majanga haya. Lakini cha ajabu ni kwamba Tanzania kama nchi inajadiliana na nchi nyingine kuwa na Sera moja ya Fedha, wao wanataka hiyo nchi moja iwe na sera mbili tofauti za fedha, Barazil na China zinafikiria kuwa na fedha moja ili kukuza biashara, na uchumi, wao wanasema fedha ya pamoja inadhoofisha uchumi; sijui hawaelewi hata kinachoendelea duniani?

Kwenye Blue, msingi mkubwa wa Muungano ni uraiya vinginevyo unakuwa si muunggano bali ushirikiano wa kibiashara, (vilevile hata kama ni ushirikiano wa kibiashara, kupunguza masharti ya uraiya na kuufanya kama ni mmoja ndio hitajio kuu la kufikia lengo la ushirikiano) sasa wao wanasema hili hapana; sasa hata huelewi wanataka nini? Maana sisi watanganyika tuko wazi kabisa, ima daini kura ya maoni ya kujitoa katika Muungano completely au bakini tutakavyo, sio blabla za sokoni. Hata hivyo, kwa hoja hii, muanze maandalizi ya kuwapokea watu wenu, msije kusema mmeshtukizwa muda mfupi ujao.

Hiyo ya mwisho, ni umbumbumbu wa kutoelewa tu mambo ya ushuru wa bidhaa, maana hata haieleweki. Zanzibar by nature ni import-based country, haina production ya kutosha na ina population ndogo, hivyo iwapo itakuwa na ushuru wake na lets say kuweka kuwa juu sana, itaumiza tu watu wake na Tanganyika haitaumia kwa sababu ni nchi kubwa by production and consumption (Small& large country tariff analysis case). Na wakiweka kuwa wa chini sana, bidhaa hazita-flood kwa sababu hakuna population kubwa ya ku-absorb all imported commodities na itakuwa iko na taratibu tofuati za ushuru na Tanganyika hivyo hakutakuwa na chance ya kuuzia Tanganyika bidhaa zilizokuwa imported kupitia Zanzibar(Kutakuwa na kulipia kodi mara mbili) na hivyo automatically, wafanyabiashara hawatakuwa na sababu ya kushushia mizigo yao Zanzibar na kisha kusafirisha Tanganyika; kwani ni hasara, gharama na kupoteza muda. Jipangeni mdai kura ya maoni kuvunja Muungano ndiyo suluhu ya kudumu ma-Akhiy zangu.
Hapo katika red sio kweli umoja wa safafu na sera za pamoja ninasaidia kuinua uchumi, angalie EURO ilivyo ziangusha uchumi nchi za Europian Union ! Katika nchi za ulaya UK peke yake iko stable kutokana na sarafu ya na uchumi wake pamoja na ushuru. UK haikungia kwenye muungano wa EU mzima mzima kutokana na kujiwekea ngao kiuchumi, na sasa yupo katika harakazi zake za kujitoa kabisa, angalia UGIRIKI ilivyo anguka kiuchumi ? Na katika nchi za EU ilikuwa ipo juu sana kiuchumi.

Nawakilisha.
 
Ghibuu, usiseme kwa ushabiki au ufikiriavyo. Kapitie tena historical background ya Umoja wa Ulaya halafu uje ueleze kilichotokea na kinachoendelea. Na kapitie historia ya UK na Umoja wa Ulaya ndio utajua. UK iliwahi kuambiwa haiwezi kujiunga na EC kwa kuwa uchumi wake ni "too low" unakumbuka? Ujuwe tu ya kwamba sababu kubwa ya UK kutokuwa member wa Sarafu moja kwa vile UK ni "world centre on financial market" hivyo inaamni kutumia Euro kungeharibu status yao ya kuwa kituo kikuu cha soko la fedha duniani kwa vile ingekosa financial policy control! Je Zanzibar ina sifa hiyo? Kuhusu Ugiriki siyo kwamba kuingia Euro ndiko kumeangusha uchumi wa Ugiriki nyie watu muelewe vizuri. Kimsingi Ugiriki imefaidika sana na EU vinginevyo hali ingekuwa mbaya. Ni kwamba, Ugiriki ni nchi inayoendeshwa kiujanjaujanja kwa wananchi kutopenda kutofanya kazi, kutolipa kodi na kupokea pension kubwa (Nadhani ndiyo inayoongoza duniani). Wafanyabiashara wake wengi ambao wa meli wamesajili nje ya Ugiriki kwa hiyo Serikali ya Ugiriki haipati mapato ya kutosha hali iliyoilazimu kukopa sana katika mabenki na kuficha kiwango cha deni la Taifa (ilicheza na takwimu ili kuweza kuingia EU na kuendelea kukopeshwa). Kilipoingia chama chengine cha siasa kikatoa takwimu za kweli za deni la Serikali (Public debt) na ikaonekana deni ni kubwa kiasi cha Taasisi za kifedha kukataa kuendelea kuikopesha Serikali kwa kupandisha riba, Hivyo Serikali ikashindwa kujiendesha. Ndipo EU ikawasaidia kwa kutoa fedha chini ya mfuko wa Ulaya ulioanzishwa kwa ajili ku-restore uchumi wao (Ni nani angewapa kama wasingekuwa kwenye EU). Masharti ya EU ni pamoja na ku-run Austerity measures (kuongeza makusanyo ya kodi, kupunguza matumizi ya Serikali). Kwa kufanya hivyo maana yake wananchi lazima wafunge mkanda kitu ambacho hawataki kwani lazima hali yao ya kimaisha iwe mbaya mwanzoni ndipo wanaishinikiza Serikali yao ijitoe ili waendelee na maisha waliyozoea!!!! Kimsingi member wengi wa EU wanachangiwa fedha badala ya kuchgangia ili kuinua uchumi wao walau ulingane kwani ni kigezo kimojawapo kweny ushirikiano wa kama EU. Hizi hoja kazitolee Mtendeni ndio utaeleweka siyo hapa JF. Karibu tena ujibu na zile hoja nyingine 2 mnaozitaka kwa mujibu wa wasilisho lako na post yangu hapo juu.
 
Zinedine usihangaike na Wazanzibar, hawajui wanachokitaka.
 
Back
Top Bottom