RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes leo imeanza vibaya mbio za kuwania kombe la CECAFA Chalenji katika michuano inayohusisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na kati, iliyoanza leo nchini Ethiopia.
Katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo, Zanzibar Heroes imecheza na Burundi ukiwa ni mchezo wa kundi B na kuchapwa bao 1-0 lililofungwa na Didier Kavumbangu dakika ya 39.
Matokeo haya yanaiweka Zanzibar katika wakati mgumu kwani italazimika kushinda michezo yake miwili iliyobaki ili kutinga robo fainali.
Katika kundi hilo, pia kuna timu za Kenya na Uganda ambazo Zanzibar itakabiliana na zo katika medhi zinazofuata.
Mechi inayoendelea hivi sasa ni kati ya wenyeji Ethiopia dhidi ya Rwanda.
Ethiopia na Rwanda ziko kundi A pamoja na Kilimanjaro Stars na Somalia.
Kilimanjaro Stars itacheza kesho na Somalia.
Chanzo: EATV