Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza kuifuta usajili wake mara moja meli ya EAGLE (IMO No. 8203074) kufuatia taarifa za kukamatwa kwa chombo hicho nchini El Salvador kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya.
Kulingana na taarifa iliyotolewa Februari 27, 2026 na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar, meli hiyo inadaiwa kuwa ilikuwa inapeperusha bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Usajili wa Meli za Kimataifa wa Zanzibar (TZIRS). Taarifa za kukamatwa kwake ziliibuka Februari 17, 2026, kupitia mamlaka za Jamhuri ya El Salvador na vyombo vya habari vya kimataifa.
Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), ikitekeleza wajibu wake kama Dola ya Bendera (Flag State), imechukua hatua zifuatazo tangu Februari 18, 2026: kufuta usajili wa meli ya EAGLE ambapo imeondolewa rasmi kwenye rejista ya meli za Zanzibar, serikali imewasiliana na Jeshi la Polisi la Kimataifa (INTERPOL) kwa ajili ya uthibitisho wa kina na ushirikiano wa kiuchunguzi, na kuanzisha uchunguzi wa kisheria dhidi ya wahusika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Usafiri Baharini Zanzibar.
“Pamoja na hayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina sera ya kutovumilia kabisa matumizi mabaya ya Bendera yake kwa shughuli zozote za uhalifu wa kimataifa, ikiwemo: usafirishaji wa dawa za kulevya, biashara haramu ya binadamu, uvunjifu wa vikwazo vya kimataifa na uhalifu wa kifedha au wa kimazingira baharini”, imeeleza taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa iwapo tuhuma hizi zitathibitishwa, uwajibikaji utakuwa wa watu binafsi au wamiliki wa chombo husika, na si wa Mamlaka ya Bendera, kwa mujibu wa misingi ya sheria za kimataifa.
Hata hivyo, Serikali imeeleza utayari wake wa kushirikiana na Jamhuri ya El Salvador kupitia njia rasmi za kidiplomasia ili kupata ukweli wote wa tukio hilo. SMZ imehakikishia jumuiya ya kimataifa kuwa TZIRS inaendeshwa kwa taratibu madhubuti za uhakiki wa wamiliki halisi wa vyombo (beneficial ownership verification) na ufuatiliaji wa utiifu wa sheria za kimataifa (UNCLOS, SOLAS, na MARPOL).
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza kuwa inasimamia kwa umakini na weledi mkubwa Usajili wake wa Kimataifa wa Meli na itaendelea kuchukua hatua kali.
Pia, Soma
- El Salvador yakamata tani 6.6 za cocaine, meli iliyobeba unga ina bendera ya Tanzania!
- Gerson Msigwa: Meli iliyokamatwa na Cocaine El Salvador imesajiliwa Zanzibar, na tayari imefutiwa usajiliKwani bendera iliyotumika ilikuwa ya Zanzibar au ya Tanzania?, mbona wanajichanganya hao wakati bendera ya Zanzibar si inajulikana.
kwenye bendera ya tanzaia wao hawapo?Hizo meli zinazosajiliwa Zanzibar zitumie bendera ya Zanzibar. Kwa nini watumie bendera ya Tanzania wakati wana bendera yao?
Wahusika wa huo mzigo wa cocaine wapo humu humu nchiniUpande fulani huko nje unaongoza kwa kufanya biashara hiyo
Ova
Waliyokamatwa watabinywa watasema destination ya meli hiyo ilikuwa inaenda wapi!Wahusika wa huo mzigo wa cocaine wapo humu humu nchini
Unamaanisha Tanganyika ama? Maana Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Nadhani hii ni kujisafisha tu lakini damage tayari ni kubwa tena kwa Tanzania sio Zanzibar, Tanzania ndio anawajibika katika hili.
Balaa kweli kweli
Shida sio kwamba haina market TZA.. shida ni pale TZA inatumika kama safe route kwa biashara Haramu ikiwemo hizi za madawa na human trafficking...mara ngapi wa Ethiopia wanakamatwa wakiwa wanapita kwenda south Africa. Na hao ni wachache je, ni wangapi wamepita salama TZA pasipo kushtukiwa?Waliyokamatwa watabinywa watasema destination ya meli hiyo ilikuwa inaenda wapi!
Ila kwa tz cocaine haina market sana kama heroin
Ova
Aisee, 🇹🇿Pamoja na hayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina sera ya kutovumilia kabisa matumizi mabaya ya Bendera yake kwa shughuli zozote za uhalifu wa kimataifa, ikiwemo: usafirishaji wa dawa za kulevya, biashara haramu ya binadamu, uvunjifu wa vikwazo vya kimataifa na uhalifu wa kifedha au wa kimazingira baharini”, imeeleza taarifa hiyo.
Hizo yard za magari znazomklikiwa na mapaka huko nyumbaniShida sio kwamba haina market TZA.. shida ni pale TZA inatumika kama safe route kwa biashara Haramu ikiwemo hizi za madawa na human trafficking...mara ngapi wa Ethiopia wanakamatwa wakiwa wanapita kwenda south Africa. Na hao ni wachache je, ni wangapi wamepita salama TZA pasipo kushtukiwa?
Mkuu mara ya mwisho kusikia jina Tanganyika katika jambo lolote lile ni lini?Unamaanisha Tanganyika ama? Maana Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.