Zanzibar yaizidi JNIA kwa idadi ya wageni wanaoingia nchini

Zanzibar yaizidi JNIA kwa idadi ya wageni wanaoingia nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Uwanja ndege wa AAKIA mwaka 2021 ulipokea wageni wa kimataifa 732,000 ukifuatiwa na JNIA uliopokea wageni 604,000 wa kimataifa, ikiwa ni tofauti ya wageni 128,000.

Ripoti ya takwimu za kitaifa (Tanzania in figures 2021) inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaonyesha kuwa uwanja huo kwa miaka mitatu (2017 hadi 2019) AAKIA ilikuwa inapokea baada ya mlipuko wa Uviko-19 ulioathiri dunia nzima kuanzia mwaka 2019, mambo yamebadilika.

Uwanja huo miaka ya 2020 na 2021 uliongoza kwa idadi ya abiria wa kimataifa waliotua na kuipiku JNIA.

Uwanja unaofuatia kuingiza wageni wengi ni wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ulioshika nafasi ya tatu kwa kupokea wageni wa kimataifa 150,000 huku viwanja vingine nchini kwa ujumla wake vikipokea wageni wa kimataifa 4,000 kwa kipindi cha mwaka huo.

“Wakati ule wa Uviko-19 watalii wengi Tanzania walikuwa Zanzibar, kwa hiyo ndege kutoka mataifa mbalimbali zilienda kuwachukua raia wake, hii inaweza kuwa imesaidia kuongeza idadi ya watalii Zanzibar baada ya janga hilo kuisha,” alisema Juma Fimbo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya usafiri wa anga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Masoko ya Utalii Zanzibar, Mohamed Mansoor alisema takwimu hizo zinaonyesha jinsi utalii wa Zanzibar ulivyokua kutokana na ndege nyingi kubwa kuutambua uwanja huo, ambao hivi sasa unapokea ndege nyingi.

“Kuongezeka kwa wageni wa kimataifa Zanzibar ni ishara kuwa shughuli za utalii zimeongezeka na pia ndege kubwa kutoka maeneo mbalimbali ya dunia zinaweza kutua AAKIA tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Mansoor.

“Tunadhani wageni wengi waliokuja Zanzibar kupitia uwanja huu wa ndege (AAKIA) watakuwa ni watalii kwa sababu karibia asilimia 30 ya Pato la Taifa la Zanzibar linachangiwa na shughuli hizo,” aliongeza waziri huyo.

Takwimu hizi zinabainisha kuwa karibia nusu ya abiria wa kimataifa (asilimia 48.8) walioingia nchini mwaka 2021 kupitia usafiri wa anga walishukia Zanzibar kwenye uwanja wa AAKIA.

Katika mwaka 2020, abiria wa kimatifa waliowasili katika viwanja vya ndege nchini walikuwa 943,000, idadi ambayo iliongezeka hadi milioni 1.5 mwaka 2021.

Kutokana na ongezeko hilo la wageni, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali ya kuweka miundombinu na huduma kwa wageni hao.

Miezi minne iliyopita, Waziri wa Utalii na Malikale wa Zanzibar, Simai Mohammed Said alifanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Hussain Ahmad Al Homaid kwa ajili ya kudumisha usafiri wa anga baina ya nchi hizo, hasa wakati wa Kombe la Dunia litakalofanyika November nchini Qatar ili kusaidia kuongeza utalii nchini.

“Tumezungumza kuhusu njia za kuwapata baadhi ya watalii ili wabaki Tanzania wakati na baada ya Kombe la Dunia kuanza, ili waweze kutazama mechi Doha na kurejea Tanzania kama makazi yao makuu wakati wote wa mashindano,” alisema Simai.
 
Kuna haja ya kupunguza bei ya E-Visa ili kuhamasiha, Biashara ni ujanja ndugu zangu Wataita.
 
Kwani nyie mnatakaje sasa? Watalii wa Zanzibar walazimishwe kwenda bara ili idadi ya watalii wa bara iongezeke?
 
Hizi comments za kuonyesha nani ni nani zimeshamiri siku hizi. Mnazitoa kwa faida ya nani? Wakishukiwa Zanzibar, Dar es salaam Kilimanjaro au popote yote ni heri tu.

Zanzibar ni maarufu kwa utalii wa fukwe. Ni wazi wageni wengi wanaoingia kwa ajili ya mapumziko watakwenda Zanzibar moja kwa moja. Kingine ni bei ghali ya kutembelea mbuga za wanyama. Unajua ili mgeni aingie Gombe National Park analipia $118 kama entrance tu?

Hii dhana ya kuweka kodi kubwa inalighalrimu taifa. Ngorongoro haendi mtalii wa budget ya wastani. Kodi kila mahali na bado wanatamani kuongeza tu.

Tanzania ina nafasi kubwa sana ya kukuza utalii na kuongeza watalii
 
Lazima waizidi...sasa we unataka watali waje dar waende kidimbwi

Ova
 
Mleta mada ninashindwa kumuelewa zaidi ya kwamba naona kama ni mbaguzi wa kikanda ama mtu mwenye kupenda na kutetea migawanyiko zaidi ya umoja na muungano,
maana anajionesha kwamba angependelea wageni wanaoingilia Zanzibar waingilie wapi? na anakosea sana anaposhindwa kutambua kwamba zanzibar ni sehemu ya Tanzania kama ilivyo Dar es salaam ama kilimanjaro na sehemu nyinginezo hivyo haijalishi kama mgeni kaingilia ama katokea wapi…na hili la wageni wangapi wameingilia wapi halipaswi kuwa sehemu ya mjadala humu,mgeni anaingia pale anapopata huduma aliyoifuata hivyo ameingilia zanzibar kwa sababu beach ama fukwe zipo Zanziba,anayeingilia kilimanjaro ni kwa sababu ni karibu na mlima ama mbuga anazohitaji kutembelea hivyo huwezi hamisha bahari ukaipeleka mwanza ama singida vile huwezi hamisha mlima ama mbuga za wanyama sehemu zilipo ila kizuri ni kwamba mapato yanayotokana na wageni hawa kwa yanawafaidisha watanzania wote kwa namna moja ama nyingine.
 
Back
Top Bottom