Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Wizara ya Afya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya 29 wa #COVID19 na kufanya idadi ya maambukizi visiwani humo kufikia 134. Wagonjwa wote waliotangazwa leo ni Watanzania
Pamoja na ongezeko hilo, Wizara pia imesema wagonjwa wengine watano wamefariki dunia na 11 wamepona na kufanya idadi ya waliopona kufika 16
Waliolazwa katika vituo vya kutolea huduma ni 41 na hali zao ni nzuri. Utaratibu wa kuwatibia nyumbani wagonjwa wenye dalili chache na ambao hawana matatizo mengi ya kiafya unaendelea na sasa wagonjwa 72 wanatibiwa nyumbani
Wizara hiyo imeendelea kuwahimiza wananchi kuvaa barakoa wanapokuwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu