Shirikisho la soka Afrika (CAF) limeivua uanachama Zanzibar miezi minne tu baada ya kupewa.
Rais wa CAF, Ahmad amesema kuwa Zanzibar, ambayo ni sehemu ya Tanzania haikutakiwa kukubaliwa kama mwanachama wa 55 wa shirikisho hilo.
"Walikubaliwa uanachama bila uchunguzi wa kina wa sheria ambazo zipo wazi kabisa," alisema Rais, Ahmad.
"CAF haiwezi kusajili Shirikisho mbili tofauti kutoka nchi moja."
FIFA walikataa kuisajili Zanzibar baada ya CAF, iliyokuwa chini ya rais mtangulizi wa Ahmad, Issa Hayatou, kuikubalia Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF.